Jinsi ya kununua BUM KUBAM DVD ya NICK WA PILI Angalia hii video

Kabla ya kucheck hiyo video 

MFUMO RAFIK(CODE NAMBA) WA USAMBAZAJI MUZIK NA FILAMU TANZANIA

Ukitaka kununua bum kubam dvd ya nikk wa pili, Unaingia  Mpesa kwa kupiga *150*00# , kisha unachagua lipa bili yako kwa kuchagua namba 4, kisha unaweka namba ya kampuni yetu ambayo ni 212121, kisha unaweka kumbukumbu namba ya malipo ambayo ni jina la dvd ambayo ni Bum Kubam , kisha unaweka kiasi 4000, na kufata maelekezo. Baada ya malipo kukamilika,mda mchache baadaye utapokea meseji kutoka fichuka ambayo itakupa code namba ya hiyo dvd uliyonunua. 

  Baada ya kupata code namba utatakiwa kwenda kwa wakala wa fichuka aliye karibu nawe ambaye atahakiki code namba yako na kukupa DVD/CD , pia utapata maelekezo ya meseji ya njia rahisi ya kufahamu wakala wa karybu alipo. Kwa maana nyingine DVD/CD haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi.
FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
Ni mfumo rafiki kwa sababu ni mfumo unaopunguza vichocheo vya wizi wa kazi za wasanii kwa kufanya yafuatayo,

1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo huu ambapo atakua na akaunti yake ambapo ataweza kuona idadi ya nakala zote alizouza na mahali zilipouzwa.

2. Kwa sababu jamii itafahamu kwamba bidhaa hii haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi na anayefanya hivyo ni mwizi, itazuia wauzaji  wezi kuuuza bidhaa hii. Muuzaji anatakiwa ahakiki code namba sio kupokea  pesa.

3. Bidhaa yeyote inayonunuliwa kupitia mfumo huu ni lazima iwepo kwnye database yetu, kama unayo  bidhaa na haipo kwnye database yetu ni dhahiri kwamba umeshiriki katika kumuibia msanii na hatua za kisheria zitachukuliwa,

4. Msanii ana uwezo wa kufahamu kwa majina kila aliyenunua kazi yake na mda alionunua na anaweza pia kuwasiliana na wanunuzi kama atahitaji kufanya hivyo.

5. Kupitia mfumo huu, kazi ya msanii itakua inapatikana kiurahisi kama vocha dukani,  kwa hiyo itaongeza uhitaji wa kazi ya msanii na kupunguza mawazo ya kunakili kazi ya msanii.

6. Kwa kuwa wakala hanunui bidhaa, haingii gharama yoyote bali anapata commission itaongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji.

7. Kwa kuwa pesa anafaidika  moja kwa moja na mauzo ya kazi zake, wapenzi wa msanii watapenda kushiriki katika mfumo huu kwa kumsupport   msanii na kupata mawasiliano kutoka msanii moja kwa moja.

8. Kwa kuwa itakua inafahamika idadi ya nakala zote zilizouzwa itakua ni rahisi kucontrol soko la mzik na filamu Tanzania.

Bonyeza katikati kuAngalia jinsi ya kununua wimbo huo.......

AJABU: Jamaa ataka kumuua mwanasiasa wa Bulgaria, Ahmed Dogan akiwa jukwaani akitoa hotuba

Mtu asiyefahamika aliibuka jukwaani na kumnyooshea bastora mwanasiasa Ahmed Dogan  wa nchini Bulgaria na kutaka kumuua kwa kumuelekezea kichwani na baadae ukatokea mkanganyiko na kushindwa kufanikiwa. Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Angalia video hii ujionee.....

Kati ya Video kali kutoka Mbeya, Prince Bulenge ft Zest & Jay P

Shukrani za pekee zije kwako wewe unayeendelea kutembelea www.infogramme.blogspot.com na kusupport muziki wa Mbeya na kizazi kipya kwa namna moja ama Nyingine.. Kwa niaba ya wadao wa mziki Mkoa wa Mbeya nasema ASANTEE!!

KICHUPA kingine kutoka GreenCity Shababi - Wamelewa {Video}


"KIVULI" ya Wastara na Marehemu Sajuki yaingia sokoni LEO

Filamu aliyoigiza Marehemu Sajuki na mkewe Wastara iitwayo KIVULI imeingia sokoni rasmi leo. Filamu hiyo imeandaliwa na kampuni yao Wajay Film Co. na kusambazwa na kampuni ya Steps Int.

Ingia sokoni kupata nakala yako halisi kukuza sanaaa ya Tanzania.

WALTER: Talkin' After Ushindi


Chamillionaire: "I'm Comming"

Rapper Chamillionaire yupo tayari kurudi na Project Mpya ya Elevate. Fahamu kuwa Chamillionaire ameka kimya kwa miaka 5 Bila wimbo kwenye radio wala video.

Rapper huyu from Houston alitangaza project hii kwenye facebook page yake nakusema, FEB 12th on www.chamillionaire.com. The first 500 copies will be autographed and each autographed copy will be numbered…

COMING SOON: Ki-UtuUzima Video


HEMEDI: Video ValentineDay

Hemed Suleiman baada ya kuachia ngoma yake mpya mwaka jana inayokwenda kwa jina la Going Crazy kutoka B hits, sasa basi anatarajia rasmi kuachia video yake mpya siku ya tarehe 14 Valentine Day.Kaa tayari kwa ujio huu mpya kutoka kwa PHD.

COMING SOON: FA - The Finest



Kama wewe ni shabiki wa Mwana FA basi huu ndiyo ujio wake mpya 2013 ambao anatarajia kuuachia siku za hivi karibuni kaa tayari kwa ujio kutoka kwa msanii huyu.

HUU NDIO WIMBO WA WABABA MTUKA, NO 3 EBSS 2012

Wababa Mtuka mshiriki na mshindi wa tatu wa Epiq BSS 2012

INTRO:                                                  
Ema the boy mmh! mmh!
VERSE  1
 Kiukweli sina hata la kusema my wife
Ajali nyingi za mapenzi nilopata unajuaaa  

ooh! unajuaa ! machozi niliyoliaa!
Usiku na mchana usibhabhakulunjalibhan
Baby usije kata tamaaa Vulu vulu vulu!

 CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

VERSE 2.
Iye he!  Kama mapenzi ni kung'ang'ana { Basi ng'ang'ana 

Na kama mapenzi unajua sana { Basi kazana
Mukikiki, nasijawahi,mapenzi yako sioni tena
Omwanajhonteme,nakupenda Habibi uhibuk { Nakuwaza}
Naweza wa hatakwanaino { Hata kwanaino}
Halikosi na mikingamo { Nami kingamo}
 Nawahi wahi,watusome,pia wajue,wanipa raha
Ninachotaka,jitulize,jiwekebize, hapontafurahiiii
Ey Vulu vulu vulu.

CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

VERSE 3.
Iye he!  Zito haliwi zito kwanza mpaka lipimwe

Tabia ya mtu ni kama ngozi ukiweza fasta ivue
Nai na nai nai nai nai x2
Ukiona nyani porini najiweka Ujue na ficha mkia wangu
{ Nai na nai nai nai nai }x2
Mh uko fitifiti kwa kitikiti, Unahitihiti, kwa mutimuti
Yani huchoshi choshi, Sikoshikoshi
Nikilala shishishi,Unatishitishiii Eeeh aaaaah

CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

KUHUSU DIAMOND NA WOLPER



Diamond Amekanusha Uvumi kuwa anamahusiano ya Kimapenzi na Jaqueline Wolper Nakusema Kuwa Picha zilizo onyweshwa kwenye magazeti ni za video ya Keisha 'Nimechoka' aliyo Shirikishwa Diamond. Plantnumz amesema video shoot ya wimbo huu ilianza Miezi miwili iliyopita na kuja kukamilika wiki Mbili zilizo pita na ndio scene ya video hio inamuonyesha akiwa karibu na Wolper.
Hiki ndicho kilichoandikwa Gazetini..
Pia Diamond amesema Msichana yoyote atakaye sema ni Girl Friend wake kwa sasa Ni Muongo kwani yeye yupo single kwa sasa na hana mpango wa kutangaza Mpenzi wake atakaye mpata. Diamond Alikaririwa na sammisago.com akisema `Simba akiwa Karibu na Swala, Watu wanadhani Anamla, Ila Kuna Muda Simba Anashiba'

Darasa Ft.Winnie - NishikeMkono(Official Video)


MILLARD-MIAKA YANGU 6 NYUMA

ALICHOANDIKA MILLARD AYO KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK LEO Ni moja kati ya post zisizo na picha lakini imepata LIKES, COMMENTS na SHARE nyingi kuliko zote alizowahi kuandika.

HIKI ndicho alichoandika..(MAISHA NA MAPENZI)

"Miaka 6 iliyopita wiki kama hii ndio nilipata tuzo ya kwanza ya Utangazaji kutoka Tanzania Radio Awards, nikapandishwa mshahara toka elfu tano mpaka elfu kumi kwa wiki kwenye radio niliyokua nikifanyia kazi, sikutamani kufanya kazi nyingine japo nilikua naishi kwenye hali ngumu sana, niliahidi nitapambana ili nifanikiwe kwa hii kazi kwa sababu naamini Mungu ameweka kitu ndani yangu, nasema Amen leo nina maisha ninayoridhika nayo kabisa tena sana, Namshukuru Mungu sana kwa hilo! hii ni maalum kwa watu wangu wote wa nguvu ambao wanapitia shida, hawana kazi au wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni, wanatafuta kazi kila siku hawapati, ukweli ni kwamba SUBIRA ni kila kitu, Nidhamu ni kila kitu, Maombi ni kila kitu, Kujituma ni kila kitu! kutokakuta tamaa ndio muhimu kabisa."
Millard akiinterview na Rosee..
Kila la kheri kaka ktk kazi zako..

SHILOLE&CHILLAH - DUDU Video

Official Video ya msanii SHILOLE feat. CHILLAH. Nyimbo inaitwa DUDU na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri Shabani.

RAY C AMSHUKURU KIKWETE KWA KUSAIDIA KUPONA KWAKE

Msanii wa kike wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amemshukuru sana rais kwa kumsaidia kupona kwake leo alipopata nafasi ya kumtembelea Ikulu.
 
Ray C ni moja kati ya watu waliokuwa waathirika wa madawa ya kulevya kupelekea afya zao kuwa mbaya..
Ray C kulia akiwa na Rais Kikwete.
Kutoka kushoto ni Bibi wa Ray C, Rais Kikwete, RayC na Dada yake.

R.I.P. MZEE ELEBUWA NOLLYWOOD

Mwigizaji nguli toka nchini Nigeria Enebeli Elebuwa (65) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini India kutoka na ugonjwa wa kupooza uliompata mwaka 2011.

Alianza kuigiza mwaka 1967 na alikuwa anavutia sana akiigiza kama mfalme au 'pedeshee' na filamu nyingi ameigiza hivo.


Hizi ni baadhi ya filamu alizowahi igiza Lost Kingdom, Abuja Connection, Sensational, Dons in Abuja, The Corridors of Power, Men Do Cry, Who Will Tell The President, and Royal War.

YOUR NEW MAISHA PLUS STAR

Bereniki Kimiro ndiye ametangazwa kuwa mshindi wa Maisha Plus kwa mwaka 2012 kwa kuwashinda wenzake.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Venance Kimaro na nafasi ya tatu imekwenda kwa Justine ambaye anatoka mkoani Dodoma.

Kila la Kheri bibie na hizo Mil. 20...

ALICHOANDIKA WALTER KTK BLOG YAKE YA chilambo.blogspot.com

NAOMBA niwaahidi mashabiki wangu kuwa hivi karibuni kama MUNGU  akipenda ndani ya hizi wiki mbili (2) nitaachia ngoma yangu mpya ya kwanza Officially na naamini kama itakuwa poa kwa jitihada zangu katika hilo

Nitatoa maelezo yote ya nyimbo hiyo hapahapa kabla hata ya kuitoa kama nimetengeneza wapi na Producer gani na jua kuwa utakuwa utunzi wangu mimi mwenyewe.
Pia kuhusiana na Collabo yangu na Ben Pol, Hata kabla Ben Pol kusema kuwa anataka Collabo na mimi, Yeye ni moja kati ya wasanii ninao wakubali na ndio maana hata wimbo wake ulikuwepo katika listi ya nyimbo zangu nilizoimba FINALE.
Ben Pol akimtuza Walter siku ya FINALE
Hivyo kwa sasa naona ndoto zangu zinatimia, hivyo watu wangu wategemee ngoma yangu na Ben Pol kwani kilichobaki ni kuongea nae na kufanya kazi tuu,Jua kuwa NIKIKUPATA ya BEN POL  ni wimbo ulonifanya kuwa STAR kuliko nilivyofikilia.
Nawapenda sana watu wangu na nawaomba tuendelee kuwa pamoja katika kazi zangu kwani jua kabisa kuwa hakuna MIMI bila WEWE.

CHEKA NA ABBY

Zuzu mmoja alipita sehemu flani akakuta
watoto wanacheza, akawadangaya wale
watoto,
"Nyie nendeni kule kuna chakula
kinagawanywa." Wale watoto kuskia hivyo wakatimua
mbiooo! Zuzu kuona watoto wametoka mbio
akajisemea moyoni,"Mbona wanakimbia
mbio sana labda kuna chakula kweli." Naye akaanza kukimbia ili kuhakikisha kama
kipo kweli.....

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA