MPYA KUTOKA KWA WASTARA HII HAPA:

Maisha yake yalikumbwa na mikasa mbalimbali kutokana na kuugua, mume wake Sajuki kufariki dunia pamoja na mikasa mingine ambayo ilimkumba kwa miaka ya hivi karibuni.

Check hii Picture: Hii ni zaidi ya Cartoon +=%#@^


RIP S.A.C.P James Kombe,

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Video: Godzilla ft. Walter "THANKS GOD" Official

Madam Ritha: Msiogope Maadui, ameitoa kwa D. Carnegie

Katika UKURASA wake wa FaceBook, Madam Rita ameandika Hiviii..
"Usiogope maadui ambao wanakushambulia. Ogopa marafiki ambao wanakusifia. " - Dale Carnegie

STRESS za Mapenzi kwa Diamond Plutnumz, Zinamfanya aendeleekuandika Ujinga Mitandaoni, Check kama hii


Morning watu wangu wa kweli..!!Sote tunakubaliana na ukweli kuwa mapenzi yanaumiza sanaaa.

siyo?so nataka nione likes na coments za wale walio experience maumivu ya mapenz ukicoments uliumizwa kwa kisa kipi
na ni wimbo wangu upi ukiuskiliza unakufariji ama unakukumbusha ulivyoumizwa.
na mlioumiza wenzenu mwaweza shiriki pia.
twenzetu!!!!!
#WCB for life baby

BOKO HARAMU WAUA WENGINE 19, BAADA YA 80 WA JUZI

WATU 19 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno nchini Nigeria, kwenye kizuizi cha barabarani walichokuwa wameweka.
 
Wanamgambo hao, wamewaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kuwanyonga wengine 14 na baadae walitokomea baada ya kupata taarifa za wanausalama kuja eneo la tukio.

DUNIA NZIMA MTU MMOJA ANAKOSA CHAKULA KATI YA WATU 8

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa  zaidi ya asilimia 12 ya jamii ya watu duniani,  wanakabiliwa na njaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Jose Silva, ameeleza kuwa, kutokana na wastani huo, ina maana kwamba mtu mmoja kati yawatu 8 ana tatizo la ukosefu wa chakula.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, watu milioni 840 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula kwa mwaka huu ambapo idadi hiyo imepungua kutoka watu milioni 870 kwa mwaka jana.

InfoGramme: FAMILIA WAMEKUFA KWA MOTO MBEYA

WAKAZI wa Ilemi, jijini Mbeya mkoani hapa, Fadhir Said na mke wake, Lucy Said, wamefariki dunia baada ya kuungua na moto baada ya nyumba yao kushika moto na kuwaka usiku wa kuamkia leo.

Check Story ya Mtangazaji anayedai kupigwa risasi 2nduma


Mwandishi wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma, katika wilaya mpya ya Momba mkoani hapa,  Shomi Mtaki, amepigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi shambani kwake.

Kingine alichoandika Diamond kwenye Instagram kuhusu picha zake na Wema muda mfupi uliopita...

Baada ya picha kusambaa kwenye internet zikimuonyesha Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja na stori nyingine zikisema wamerudiana, Diamond amepost hii picha na kuandika.
Baada ya picha kusambaa kwenye internet zikimuonyesha Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja na stori nyingine zikisema wamerudiana, Diamond amepost hii picha na kuandika..

John Mnyika: Alichoandika FaceBook leo, uhusiana na Baraza la Vijana

Pamoja na kuzinduliwa maonyesho ya wiki ya vijana jana, ni muhimu kuhoji utekelezaji wa maazimio Baraza la Vijana yaliyopitishwa Iringa 1998.

Pili, Napenda kutakia kheri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kuzindua leo Taasisi "Confucius Institute". Ni vyema ikawa fursa ya kuchochea zaidi ya lugha na tamaduni za kichina
.

AUDIO: Hii ndio Ngoma ya DIAMOND aliyoilalamikia imevuja

SKILIZA NA DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED (Hylands)

HIKI Ndicho alichoandika Diamon Plutnumz kuhusiana na UVUMI mitandaoni juu ya MAHUSIANO yake ""I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA""


"Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada
Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu
ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu 
yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..

Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko
kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? 
Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana 
Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda
wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania.
na si kuekeana chuki zisizo nanfaida..”
”I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA."

Mzee Majuto atangaza kugombea ubunge mwaka 2015..

Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015. Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza  kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.

Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM. Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni kwa kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.

NU VIDEO: Top C "WAPI ULIPO" Comming soon JOH!!

Baada ya kimya cha muda mrefu, Msanii Top C anatarajia kuachia VIDEO ya wimbo wake mpya, Wapi Ulipo. Top C kwa sasa yupo nchini Kenya akiwa chini ya CandynCandy Records…

AmmyChiba: Mpe Support huyu dada wa Green City kwenye EBSS. Hapa ni VIDEOZ: Track yake na wakati akiongea na Infogramme Blog

VIDEO: UTAMU wa Epiq Bongo Star Search umeanza

Jumapili hii ndani ya Club BILLZ 'Chid B'


BIFU YAISHA: Man Walter na 20% Beef BASI


Kwenye ukurasa wa facebook wa Magic Fm na Channel Ten taarifa hii imetolewa hivi..
Hatimaye bifu kali kati ya msanii aliyewahi kutwaa tuzo 5 za KTMA nchini kwa pamoja na kuvunja rekodi, TWENTY PERCENT na aliyewahi kuwa Producer wake pia mshindi wa tuzo ya matayarishaji bora wa muziki nchini KTMA 2012, MAN WATER, limemalizika rasmi  kwa wawili hao kukutana na kumaliza tofauti zao. 
Man Water na Twenty Percent walikutana na wawili hao wamekubaliana kufanya kazi tena pamoja na kusahau yaliyopita.
Akizungumzia kiundani kuhusu tofauti zao Man Water alisema tatizo lilikua ni kutoelewana au kupishana kwa kauli ambazo walizimaliza na hatimaye kuweka mikakati mipya ikiwemo ya kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalumu.
Kwa upande wake 20% amesema tofauti zao hazikuwa za msingi bali ni kupishana tu kwa kauli na sasa yuko tayari kufanya kazi pamoja na Man Water.
Inaaminika kwamba kufanya kazi pamoja kwa wawili hao kunaleta mwamko mkubwa kwa washabiki wao kutokana na kuelewana katika kazi zao mbalimbali walizowahi kufanya ikiwemo kaziya Yanini malumbano, Tamaambaya, Mama Neema na nyinginezo.

Kutana na msumbufu Yohana Charles..!

AU kujadili hoja ya kujiondoa ICC


Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini Addis Ababa Ethiopia, kujadili msimamo wa bara hili kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifiu - ICC.
Mkutano huo unafuatia ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kujadili kesi zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Kwa sasa hakuna dalili kuwa kuna msimamo mmoja kuhusu ikiwa wanachama 54 wa Muungano wa Afrika waliotia saini mkataba wa Roma wanataka kujiondoa, lakini marais wa nchi hizo bado watajadili uwezekano wa wanachama 34 wa mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC watajiondoa ICC.Mwandishi wa BBC mjini Addis Aabab, Emmanuel Igunza anasema kuna dalili kuwa ombi hilo la Kenya limeanza kuungwa mkono na mataifa mengi barani.
Tangu kuanza kwa kesi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC wiki jana, na ile ya Rais Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Novemba, dalili zimeonekana kuwa wengi hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi kukandamiza waafrika.
Kikao cha dharura sasa kimepangwa kujadili swala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka kuungwa mkono katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna uwezekano wa nchi wanacahama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna nafasi ya maombi mengine kufanywa kuhusiana na hilo.

ICC yataka mwandishi wa Kenya akamatwe

Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa raia Mkenya ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kuwahonga mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Viongozi wa mashtaka walisema kuwa mshukiwa huyo Walter Osapiri Barasa ameshtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kutumia njia za ufisadi kumshawishi shahidi mmoja na mkewe kwa kumlipa shilingi milioni 1.4 au dola 16,200, ili wajiondoe kama mashahidi katika kesi hiyo.
Aidha mahakama inasema kuwa ni juu ya Kenya sasa kumkamata Barasa..

Skiliza na Download Mixing kali za Dj Speed 4rm Hylands FM Mby, So Crazzzy

Pics: Check out Kilivyonuka Mwanjelwa Mbeya


Wishes: Happy Birthday DIAMOND PLATNAMZ

Katika ukurasa wake wa FaceBook Diamond ameandika "HAPPY BIRTHDAY MIMI"

NU Audio: East U "VITA MADAWA" GreenCity UP

BONGE LA HIT: Chanty Bizzy - "GHETTO PARADISE" Audio.. Iskize na Download hapa...

TAARIFA: LIGI daraja la 4 mjini Mbeya kuanza soon


Ligi ya daraja la nne jijini Mbeya inategemea kuanza hivi karibuni endapo zoezi la kurudisha na kupokea fomu likamilika siku ya leo.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu jijini Mbeya, Watson Mwakisole, amesema kuwa ligi hiyo inatarajia kuanza tarehe 21 mwezi huu baada ya taratibu za awali kukamilika. Amezitaja timu 14 zinazotarajia kushiriki ligi hiyo ikiwa ni pamopja na timu ya Prison Junior ambayo ni timu mwalikwa.

Mwakisole ameeleza kuwa Prison Junior itashiriki ligi hiyo na endapo ikipata ubingwa itapewa zawadi isipokuwa hawatocheza ligi ya mkoa kwani hii ni kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya uhai.

Katibu huyo ameongeza kwa kueleza changamoto wanayokutana nayo kuwa ni kutokuwa na wadhamini wa ligi hiyo.

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA