Ligi ya daraja la nne jijini Mbeya inategemea kuanza hivi karibuni endapo zoezi la kurudisha na kupokea fomu likamilika siku ya leo.
Katibu mkuu wa chama
cha mpira wa miguu jijini Mbeya, Watson Mwakisole, amesema kuwa ligi hiyo
inatarajia kuanza tarehe 21 mwezi huu baada ya taratibu za awali kukamilika. Amezitaja timu 14 zinazotarajia kushiriki
ligi hiyo ikiwa ni pamopja na timu ya Prison Junior ambayo ni timu mwalikwa.
Mwakisole ameeleza kuwa Prison Junior itashiriki ligi hiyo
na endapo ikipata ubingwa itapewa zawadi isipokuwa hawatocheza ligi ya mkoa
kwani hii ni kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya uhai.
Katibu huyo ameongeza kwa kueleza changamoto wanayokutana
nayo kuwa ni kutokuwa na wadhamini wa ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment