NGASSA ALIVYOWASILISHA MILIONI 45 ZA SIMBA TFF JIONI HII

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (katikati) akiwa ameshika risiti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kulipa Sh. Milioni 45, alizotakiwa kuilipia klabu ya Simba SC. Wengine kulia ni Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto na kushoto Mhasibu, Rose Msamila. Ngassa alifungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na kutakiwa kurejesha fedha za Simba Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, baada ya kubainika alisai timu mbili, Simba na Yanga alikoidhinishwa kucheza msimu huu..

EMPIRE CHANT BIZZY & NYANDSON - REVOLUTION (OFFICIAL VIDEO)


Kenya yaapa kumsaka Samantha Lewthwaite

Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.

MSANII WA KIZAZI KIPYA MIEZI 6 JELA KWA WIMBO WA MATUSI

Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.

Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.

Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa.

MCHINA ametengeneza pua mpya katika paji la uso baada ya ajali iliyoharibu poa yake



Raia mmoja wa china, Xiaolian mwenye miaka 22 amefanyiwa matibabu ya kutengeneza pua mpya ambayo itachukua nafasi ya pua yake ambayo ilipata madhara alipopata ajali ya barabarani.


Xiaolian Ameoteshwa pua kwenye paji la uso wake baada ya wataalam kushindwa kuiponya ile iliyoharibika baada ya ajali.


Utengenezaji wa pua hiyo mpya, umefanywa kwa kuchukua sehemu ya mbavu za binadamu kwa kukatwa kwa muundo wa pua.


Madaktari wamesema mwanaume huyo anaendelea vizuri na zoezi la kuipandikiza pua hiyo mpya eneo la pua ya zamani utafanyika hivi karibuni.

WALOKUFA KENYA WAFIKIA 68, WAMAREKANI WAHUSIKA KUSHAMBULIA, Mateka wanaendelea kuokolewa

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Kenya kutokana na shambulio la ugaidi la Al Shabab imeongezeka na kufikia 68, na uokoaji unaendelea vizuri. Kundi la Alshabab limedai kuwa miongoni mwa wafuasi wakewalioteketeza shambulio hio watatu ni raiawa Kimarekani, FBI wachunguza.

Wliokufa KENYA Idadi imefikia 59, 175 Majeruhi

MWANAMKE MAJERUHI AKIOMBA MSAADA...
Idadi ya waliofariki Kenya yaendelea kuongezeka.... katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabab.... Kwa mujibu wa serikali watu 59 wamefariki sasa na wengine 175 kujeruhiwa. Zaidi ya elfu moja wameweza kuokolewa......

Video: SHAMBULIO LA KENYA. Vifo 39, 150 Wajeruhiwa

Raisi Uhuru Kenyatta athibitisha vifo 39 na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa na waliofanya shambulio ni Al Shabab.

PICHA&Maelezo: SHAMBULIO LA KENYA. Vifo 39 vyathibitishwa, Al shabab wakiri kufanya shambulio, 150 Wajeruhiwa

Afisa mkuu wa Alshabaab, amefahamisha jamii kwa Twitter kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.

Kwa mujibu wa Afisa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.

Raisi Uhuru Kenyatta athibitisha vifo 39 na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa na ameongeza kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.

Taarifa hiyo Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakuya..

Dayna Nyange amekwangua ngozi ya mwili wake na kuwa Mweupeee


KABLA                                                        BAADA
Inasemekana Eti HitMaker wa Nivute Kwako Dayna Nyange amekwangua ngozi ya mwili wake na kuwa Mweupeee kama Karatasi, Tazama Picha na uskize alichojibu baada ya kuulizwa na Dalali Mpekuzi Gossip Cop wa Clouds FM.........

OFFICIAL AUDIO: Rich Mavoko "ROHO YANGU"

Wabunge wa Nigeria wapigana bungeni, Chama tawala cha PDP kimekuwa kikikumbwa na mgogoro wa ndani kwa muda sasa


Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake.

Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.

Mgogoro inasemekana ulianza baada ya mwenyekiti wa mrengo wa wabunge waliojiondoa kutoka kwa chama tawala, Kawu Baraje, kuingia bungeni akiandamana na magavana wanaomuunga mkono.

Inaarifiwa spika wa bunge la waakilishi ,Aminu Tambuwal, aliambia wabunge kuwa Baraje aliomba ruhusa kuwahutubia wabunge wa mrengo wake kabla ya bunge kuanza vikao vyake.
Lakini kuwepo kwa wabunge hao bungeni kuliwaghabisha mno wafuasi wa chama tawala, PDP,kiasi cha kuzuka sokomoko bungeni kati ya pande hizo mbili na kumlazimisha bwana Baraje kukatiza hotuba yake kutokana na kelele bungeni.

Chama tawala PDP kina wabunge wengi zaidi bungeni wakiwa 23 kati ya wabunge wote 36
Aidha chama hicho kimetawala Nigeria tangu kupata uhuru mwaka 1999 lakini hivi kribuni kimezongwa na migogoro ya ndani ya chama pamoja na kukabiliwa na upizani wenye ushawishi.

Wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mwaka 2015, lakini wadadisi wana wasiwai ikiwa chama tawala kitakuwa kimesuluhisha migogoro yake, huku kikikabiliwa na upinzani mkali.

Mgogoro huu umekuwa ukitokota kwa miezi kadhaa huku baadhi ya wabunge wakitofautiana kuhusu ikiwa Rais Goodluck Jonathan aidhinishwe na chama kugombea urais kwa mara nyingine wakati kuna wanasiasa wengine wanaotaka kugombea urais.

Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa Nigeria kurushiana ngumi bungeni.

Kutoka Polisi Mbeya: MAKALA YA ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MICHEZO MKOA WA MBEYA


Katika maisha ya kila siku ya binadamu suala la ulinzi na usalama wa mali na maisha ni muhimu sana. 
 
Binadamu huishi kwa kutegemeana basi ndivyo ilivyo hata katika suala la ulinzi wa mali na maisha yetu. Unaweza kujiuliza je,ni nani mwenye jukumu la ulinzi?je,ni mimi au wewe? Au ni sisi sote?

Basi katika miaka ya hivi karibuni Jeshi la Polisi Nchini limeendeleza dhana ya ulinzi shirikishi na ulinzi jirani kwa lengo la kushirikisha jamii kwa karibu zaidi katika suala zima la ulinzi na usalama. Zana hii imekuwa ikitoa fursa kwa jamii na wadau mbalimbali kutoa taarifa za kuzuia uharifu hali inayofanikisha kudhibiti vitendo hivyo.

Ni wazi kabisa kuwa kila mmoja wetu ana jukumu la kushiriki katika ulinzi.Ushirikishwaji huu wa wananchi katika kuzuia na kudhibiti vitendo vya uharifu ni mpana zaidi, kwani vitendo vya uvunjifu wa amani na utovu wa nidhamu si vya kuvumilika katika jamii. Kila mmoja wetu anapaswa kujua nini cha kufanya pale anapoona vitendo ambavyo si vya kiungwana vikitendeka.

Katika siku za hivi karibuni hususani  katika mechi za ligi kuu Tanzania bara kumekuwa kukitokea vitendo ambavyo si vya kiungwana wala kinidhamu katika mchezo wa mpira wa miguu. Vurugu mbalimbali kutoka mashabiki wa timu zinazoshiriki ligi kuu zimevuka mipaka kwani imefikia hatua hata ya kurushiana mawe.Katika mechi ya hivi karibuni kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga mechi iliyofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kulitokea vitendo visivyo vya kiungwana katika medani ya michezo.

Ikumbukwe kuwa suala la ulinzi katika sehemu mbalimbali ni jukumu letu sote. Kila mmoja wetu awe mlinzi wa mwenzake katika kuhakikisha amani na utulivu vinachukua nafasi yake katika michezo ili kwa ujumla wananchi wapate burudani. 

Vurugu na vitendo visivyo vya kimichezo vina athari kubwa si tu kwa timu bali hata kwa mashabiki na wananchi wa mkoa husika kwani inapotokea timu kufungiwa kutofanya michezo yake katika uwanja wa nyumbani ni athari hata katika shughuli za kiuchumi pamoja na kuua mapato ya mlangoni. Pia vurugu kama hizi ni athari pia katika shughuli za uwekezaji na kuzuia upatikanaji wa fursa ya ajira kwa wananchi.

Yapo mapendekezo mbalimbali ya wananchi juu ya suala hili la kudhibiti vurugu katika michezo. Itambulike kuwa ni suala la kila mwananchi kwani kama kila mmoja wetu ataona umuhimu wa kutoa taarifa pale anapotilia mashaka mtu/watu kwa vyombo vya ulinzi na usalama, basi suala hili tunao uwezo wa kulidhibiti na kulimaliza kabisa.Kila mwananchi atoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kudhibiti na kutokomeza vitendo vya vurugu uwanjani na katika michezo kwa ujumla.

Pengine kwa sasa ni muda muafaka kwa uongozi wa timu pamoja na shirikisho la soka nchini ni kuliangalia suala hili kwa kina zaidi ili kujiepusha na madhara makubwa zaidi. Kuwepo na adhabu kali zaidi kwa timu itakayo shindwa kuwadhibiti mashabiki wake dhidi ya vitendo visivyo vya kimichezo.

Ni imani yangu kuwa kila mwanamichezo na wadau wote wa michezo watashiriki kikamilifu kuzuia na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale waonapo dalili za vurugu kutoka kwa mtu au  kikundi cha watu kikipanga njama za uvunjifu wa amani katika michezo hasa mechi za ligi kuu zinazoendelea.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Kamishina msaidizi, DIWANI ATHUMANI anawakumbusha mashabiki na wadau wote wa michezo kuwa “michezo ni uchumi, michezo ni burudani, michezo ni upendo/amani na kila mmoja wetu aone kuwa ana kila sababu ya kutekeleza hili”

HIT Video: Chant Bizzy feat. Ammy Chiba - Acha Nifanye [Official Video] Green City Stand UP!


NU Video: Lil Stiggar ft Chris Daniel - Stress Free {Official HD Music Video}


UWOYA aapa kufa na kupona, kupambana na SHIGONGO baada ya kutoa siri nzito baina yao



Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya, ameapa kutoa siri kubwa inayofanya Mkurugenzi wa magazeti ya Udaku, Eric Shigongo, kumchukia na kitendo kinachopelekea kumchafua kila leo katika magazeti hayo.

Akilalamikia suala hilo ktk post yake aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii wa instagram, amesema kwa anaye muamini ameapa kufa na kupona kupambana na Shigongo ikiwa ni pamoja na kutoa siri nzito inayofanya amchafue.

“Ipo siku nitaongea ukweli kuhusu Shigongo na ushahidi ninao na nipo tayari kupigana nae hadi tone langu la damu la mwisho” Alisema hayo Uwoya na mengine mengi.
Picha hapo chini ni jinsi uwoya alivyotoa malalamiko hayo ambayo watu wengi wametafsiri kuwa kulikuwa na kuombana MAPENZI kati yao.

MPYA kutoka kwa Mike T, ktk Facebook Page yake

Mike Tee ni moja kati y watu maarufu Tanzania wanaoweka Funny Post katika page zao za Face book, ikiwa ni pamoja na Masanja mkandamizaji Jana usiku Mike Tee aliandika kama unavyoona hapo juu..

LYK Movie: Kituo cha kijeshi Marekani chavamiwa, wanne wauawa


Habari kutoka Washington zinasema kuwa watu 4 wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa baada ya mtu asiyejulikana kuvamia makao makuu ya jeshi la wanamaji mjini Washington na kuanza kufyatua risasi.

Habari zaidi zinasema kuwa mtu huyo bado hajapatikana ingawa inaaminika bado yuko katika jengo hilo.

Wakuu wa kituo hicho cha kijeshi wanasema maafisa kadhaa wamepigwa risasi na mvamizi huyo.
Polisi zaidi wamepelekwa kwenye eneo hilo huku shughuli katika uwanja wa ndege wa Reagan ulioko karibu zikisitishwa kwa muda.

Zaidi ya wafanyakazi 3000 wanafanya kazi katika kituo hicho kilichovamiwa. Kitengo hicho kijulikanacho kama Naval Sea Systems Command ndicho kinachohusika na utengenezaji, ukarabati au ununuzi wa meli za kijeshi pamoja na nyambizi za jeshi la Marekani.

Haijabainika ni vipi mtu huyo aliweza kuingia katika eneo hilo lenye ulinzi mkali.

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA