Walter Chilambo - Siachi (Audio) KIPAJI KUTOKA EpiqBSS 2012 SKIZA HAPAA


Mshindi wa EpiqBSS 2012, Walter Chilambo leo ameachia wimbo wake mpya uanaoitwa SIACHI ambao ulikuwa unasubiriwa sana na watu wake.

Kwa mara a kwanza wimbo huo aliuimba ktk tamasha la After school bash lakini hakuuachia na ameamua kuuachia leo na kuuimba kwa mara ya kwanza pale Cla=ub Maisha Dodoma kesho ktk show ya EpiqNight na EpiqStars.

Walter amesema anaamini kuwa wimbo huo ni mzuri na utapendwa kwani ni wa maadhi ya lika zote na kuwa anaamini tuu kuwa utawabamba.

“Wimbo huu nimewaandalia watu wangu ili kuwaonyesha kuwa hawakukosea kunipigia kura na kunifanya mshindi”

SIACHI: kuwashukuru, kuwapenda na kila kitu kizuri.. DOWNLOAD NA KUUSIKILIZA HAPO..

Oscar Pistorius: AMUUA MPENZI WAKE

Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini Pretoria.

Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi, Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.

Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani. Duiru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu
kushiriki michezo ya Olimpiki
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.

Another NU AUDIO: Baghdad Ft. Wababa - Mpaka lini LISTEN HERE

Baghdad                                                  Wababa

NU Hit: Q CHIEF - ACCURO

Nikki wa Pili ft. G-Nako - Bum Kubam

Video mpya kutoka kwa Nikki wa pili aliyomshirikisha G - Nako Bum Kubam itazame kupitia hapa..

KIPANYA: Catoon na InfoGramme


WALTER: Ziara hii anatambulisha Album

Picha kutoka kushoto ni Walter Chilambo mshindi wa EBSS mwaka 2012,
Awaichi Mawalla (Meneja mkuu mawasiliano), Nsami Nkwabi na Norman Severino.
Washiriki wa EBSS walikuwa na mkutano na waandishi wa Habari uliofanyikia Maisha Club leo hii asubuhi kuhusu Uzinduzi wa ziara yao ya kimuziki ambapo Walter Chilambo ataachia Album yake ya kwanza katika Ziara hiyo itakayoanzia mkoani Dodoma Ijumaa ya wiki hii.

Mbeya: AMUUA MWENZAKE KISA MWANAMKE WA KILABUNI


Pic: Mfano.

MKAZI  wa mtaa wa Itiji mkoani Mbeya, Daniel Mwasalemba, ameuawa kwa kuchomwa kisu na Peter Bosco wakigombania mwanamke wa kirabuni , Elizabeth Michael.

Ugomvi huo ulianza juzi wakiwa kirabuni na ukaamuliwa na wateja wengine ambapo Peter aliondoka na msichana huyo wa miaka 18 na kwenda nae nyumbani na kumpa kichapo ambapo alifanikiwa kutoroka na kurudi kilabuni ambapo alikutana na Daniel na baadae walirudi nyumbani pamoja .

Usiku wa kuamkia leo ndio Peter alirudi ktk hiyo nyumba na kuwa kuta kisha akwafungia mlango na kwenda kutafuta kisu a aliporudi akabomoa mlango na kumchoma kisu Daniel na kumsababishia kifo

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha tukio hilo na kuwa wameukuta mwili wa marehemu kando ya barabara ukiwa uchi (bila mavazi).

Jeshi la polisi linamshikilia Elizabeth kwa mahojiano kwani Peter amekimbia na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitalini.

Barnaba - Sorry (Official Video)


Kizuri: MATUMAINI ARUDI DAR, APITILIZIA HOSPITALI

Alipopokelewa Uwanjani, Kiwewe ni msanii aliyeanza nae sanaa
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Alibebwa mgongoni kuelekea kwenye Gari
ili kwenda Hospitali Moja kwa moja.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.

BABA ASKOFU THOMAS LAISER AFARIKI DUNIA HUKO ARUSHA

BABA ASKOFU THOMAS LAISER
Baba askofu thomas laiser amefariki dunia
leo jioni saa kumi na mbili katika
hospitali ya SERIAN ARUSHA.

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA