Oscar Pistorius: AMUUA MPENZI WAKE

Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini Pretoria.

Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi, Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.

Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani. Duiru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu
kushiriki michezo ya Olimpiki
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA