DULLY: Hii ndio gari yangu mpya, Pia sorry kuhusu Arafat Baunsa wangu.. Sijui chochote

Hiki ndicho alichoandika Dully Sykes ktk Website yake kuhusiana na kashfa anayokabiliwa baunsa wake Arafat Ngumi Jiwe,  "Yaani nimeumia sana baada ya kupata taarifa hizi za Arafat Ngumi Jiwe ingawa sijui kama za kweli au laa, lakini mbali na hayo ni habari chafu ambazo zinaweza kunichafua hata mimi kwa sababu huyo ni jamaa yangu wa karibu. Kitendo hicho cha kulawiti mtoto na mimi nikiwa kama baba kinanigusa kwa uchungu sana na kama ni kweli sheria itachukua mkondo wake ili kudhibiti watu wenye tabia hizo chafu".

LULU: Mtetezi wangu MUNGU Pekee, Asanteni WaTanzania mlio nami

LULU: Akiongea na waandishi kwa Huzuni baada ya kukabidhiwa
kwa Mama yake mzazi Leo  baada ya jana masuala kusuasua.
Muda mchche baada ya kukabidhiwa kwa mama yake mzazi, msanii Lulu amesema anawashukuru sana watanzania wanaoendelea kuwa pamoja na yeye na kusema kuwa anamtegemea sana Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mtetezi wake na kuwa yeye anajua Ukweli kuhusu suala linalomkabili.

LULU Apata Dhamana, Angalia picha 4 na Masharti aliyopewa

Lulu akiwa Mahakamani Leo 28/09/2013

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.

Mama mzazi wa Lulu akiwa mahakamani
kusikiliza Dhamana ya mwanaye. (Wa 2 kutoka kushoto)
Lulu akibembelezwa kupigwa picha na mwandishi mmoja wa kike
Lulu akisikiliza Dhamana yake na Masharti aliyopewa..
PICHA zote na MillardAyo.Com

EpiqBSS 2012 Competant Linias Mhaya Introduces 2 U New Song Nanje ndagukunda

Mshiriki wa EBSS 2012 Linias Mhaya ameachia wimbo wake wa kwanza unaitwa Nanje ndagukunda, angalia video hii ya Wimbo huo na Lyrics zake..

KUHUSU DHAMANA YA LULU

Jana kwenye Exclusive on millardayo.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.

Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa  zilizotolewa kwa Millard Ayo ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.

Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.

Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.

Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.

Vida ft Linex - Baba awena ( Video )


LULU KUPATA DHAMANA KESHO



Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho Tarehe 25.

Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba tangu April 2012, endelea kuipitia abrangula.com kwa stori zaidi.

NU Film: HUKUMU YANGU Kutoka kwa Dk. Chen


VIDEO: Keisha Ft. Diamond-Nimechoka

Ile picha iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha Diamond anajipaka poda ndani ya gari akiwa na msichana basi Script yake ilikuwa ya humu ndani, tizama video mpya ya Keisha akiwa na Diamonda track inaitwa nimechoka kupitia InfoGramme Blog.

Kuhusu Video hii Keysha amesema,  "Nimetumia zaidi ya shilingi za Tanzania Milioni 10 kuandaa video hii, hii ikiwa ni pamoja na malipo kwa AJ ambaye amesimamia kazi yote, video hii ilikuwa itoke muda mrefu lakini kutokana na msururu wa ratiba ya shoo za nje ya nchi nilijikuta mara kadhaa ninahirisha kushoot, nashukuru Mungu imekamilika na huu ni mwanzo wa mafanikio yangu katika mwaka huu wa 2013"

FID Q APEWA CHET MAALUM CHA HESHIMA KUTOKA UNDER THE SAME SUN

Fid Q akikabidhiwa cheti hicho na Mr. Peter Ash
Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Qubanda a.k.a Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma "Under The Same Sun" kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
 
Fid Q amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada, Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka.. "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."

Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.

MBEYA FM na PRECISION AIR

Jiandae kuwa Mmoja ya watakaotumia Vyema Dakika 90 Bora., Mbeya FM inakupa nafasi ya kutumia Dakika 90 Bora kwa Usafiri bora na wa Uhakika wa Anga kwa kutumia Precision Air..!!#Tafadhali sikiliza 89.5 Mhz Mbeya FM muda wote uwe moja ya Washindi.#Team-Mbeya FM#

TABASAMU: Infogramme na Abby


Mtoto katoka shuleni huku analia, alipofika nyumbani. Baba yake akamuuliza ''unalia nini'? MTOTO '' Nimepigwa na mwalimu na nimeambiwa twende wote shuleni''. Wakaenda shuleni na wakaingia ofisini. MWALIMU ''Karibuni, mtoto wako tumemuuliza Nairobi iko wapi kashindwa, ndio maana tumemchapa'' Baba akamgeukia mtoto wake na kumpiga vibao, akamwambia ''mpumbavu mkubwa, kila siku nakukataza kuchezea vitu vya watu hukomi, haya NAIROBI ya mwalimu umepeleka wapi'?

Mbeya: BIBI MBARONI NA LITA 9 ZA GONGO ni muuzaji kitamboo



Mfano: Uandaaji wa Gongo
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia Bibi wa miaka 62, Marry Mbuya mkazi wa Kabwe jijini Mbeya kwa tuhuma za uuzaji wa pombe haramu  (Gongo).

Polisi wakiwa katika doria walimkamata mtuhumiwa nakiwa na lita 9 za pombe hiyo ya moshi jana asubuhi akiwa maeneo ya Mwanjelwa na jitihada za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha tukio hilo na kuwaasa watu kuachana na matutumizi ya pombe hiyo kwani ni kinyume na sheria pia hatari kwa afya zao.

IZZO B: Ball Player kwa hewa

Mchonvu          Izzo B                Dozen
Uzinduzini na team Clouds Intertainment
Izzo na Quick
Hii ndio Picha ya Cover ya Track hiyo.
Huu ndio uzinduzi wa track ya Izzo B aliyomshirikisha QuickRocka na Mangwair iitwayo Ball Player ambayo imeachiwa rasmi Jumatano ya leo..  Fuata link hii kuiskiliza na kudownload..  Bofya HAPA (By Infogramme Blog)

NU Video: Hemedy PHD - Going crazy

ALISREMA ITATOKA VALENTINE DAY
Hemedy Suleiman baada ya kuachia ngoma yake mpya mwaka jana inayokwenda kwa jina la Going Crazy kutoka B hits alisema anatarajia kuachia video yake siku ya Valentine day lakini leo ipo hewani. Tizama Video hiyo kwa kubofya hapo katikati..

COMMING SOON: Izzo B Feat. Ngwair, QuickRocka - Ball Player, JumaTano Hii

Izzo B amesema kuwa Juma tano hii anaachia ngoma yake ya kwanza kwa mwaka 2013 iitwayo Ball Player ambayo amemshirikisha Mangwair na Quick Rocka, Ngoma hiyo imetengenezwa na Nahreel na Lamar.
Cover ya track hiyo iliyotupiwa na Ngwair ktk Twitter
Stay tuned kucheck Izzo anauanza mwaka vip?

Jinsi ya kununua BUM KUBAM DVD ya NICK WA PILI Angalia hii video

Kabla ya kucheck hiyo video 

MFUMO RAFIK(CODE NAMBA) WA USAMBAZAJI MUZIK NA FILAMU TANZANIA

Ukitaka kununua bum kubam dvd ya nikk wa pili, Unaingia  Mpesa kwa kupiga *150*00# , kisha unachagua lipa bili yako kwa kuchagua namba 4, kisha unaweka namba ya kampuni yetu ambayo ni 212121, kisha unaweka kumbukumbu namba ya malipo ambayo ni jina la dvd ambayo ni Bum Kubam , kisha unaweka kiasi 4000, na kufata maelekezo. Baada ya malipo kukamilika,mda mchache baadaye utapokea meseji kutoka fichuka ambayo itakupa code namba ya hiyo dvd uliyonunua. 

  Baada ya kupata code namba utatakiwa kwenda kwa wakala wa fichuka aliye karibu nawe ambaye atahakiki code namba yako na kukupa DVD/CD , pia utapata maelekezo ya meseji ya njia rahisi ya kufahamu wakala wa karybu alipo. Kwa maana nyingine DVD/CD haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi.
FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
Ni mfumo rafiki kwa sababu ni mfumo unaopunguza vichocheo vya wizi wa kazi za wasanii kwa kufanya yafuatayo,

1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo huu ambapo atakua na akaunti yake ambapo ataweza kuona idadi ya nakala zote alizouza na mahali zilipouzwa.

2. Kwa sababu jamii itafahamu kwamba bidhaa hii haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi na anayefanya hivyo ni mwizi, itazuia wauzaji  wezi kuuuza bidhaa hii. Muuzaji anatakiwa ahakiki code namba sio kupokea  pesa.

3. Bidhaa yeyote inayonunuliwa kupitia mfumo huu ni lazima iwepo kwnye database yetu, kama unayo  bidhaa na haipo kwnye database yetu ni dhahiri kwamba umeshiriki katika kumuibia msanii na hatua za kisheria zitachukuliwa,

4. Msanii ana uwezo wa kufahamu kwa majina kila aliyenunua kazi yake na mda alionunua na anaweza pia kuwasiliana na wanunuzi kama atahitaji kufanya hivyo.

5. Kupitia mfumo huu, kazi ya msanii itakua inapatikana kiurahisi kama vocha dukani,  kwa hiyo itaongeza uhitaji wa kazi ya msanii na kupunguza mawazo ya kunakili kazi ya msanii.

6. Kwa kuwa wakala hanunui bidhaa, haingii gharama yoyote bali anapata commission itaongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji.

7. Kwa kuwa pesa anafaidika  moja kwa moja na mauzo ya kazi zake, wapenzi wa msanii watapenda kushiriki katika mfumo huu kwa kumsupport   msanii na kupata mawasiliano kutoka msanii moja kwa moja.

8. Kwa kuwa itakua inafahamika idadi ya nakala zote zilizouzwa itakua ni rahisi kucontrol soko la mzik na filamu Tanzania.

Bonyeza katikati kuAngalia jinsi ya kununua wimbo huo.......

AJABU: Jamaa ataka kumuua mwanasiasa wa Bulgaria, Ahmed Dogan akiwa jukwaani akitoa hotuba

Mtu asiyefahamika aliibuka jukwaani na kumnyooshea bastora mwanasiasa Ahmed Dogan  wa nchini Bulgaria na kutaka kumuua kwa kumuelekezea kichwani na baadae ukatokea mkanganyiko na kushindwa kufanikiwa. Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Angalia video hii ujionee.....

Kati ya Video kali kutoka Mbeya, Prince Bulenge ft Zest & Jay P

Shukrani za pekee zije kwako wewe unayeendelea kutembelea www.infogramme.blogspot.com na kusupport muziki wa Mbeya na kizazi kipya kwa namna moja ama Nyingine.. Kwa niaba ya wadao wa mziki Mkoa wa Mbeya nasema ASANTEE!!

KICHUPA kingine kutoka GreenCity Shababi - Wamelewa {Video}


"KIVULI" ya Wastara na Marehemu Sajuki yaingia sokoni LEO

Filamu aliyoigiza Marehemu Sajuki na mkewe Wastara iitwayo KIVULI imeingia sokoni rasmi leo. Filamu hiyo imeandaliwa na kampuni yao Wajay Film Co. na kusambazwa na kampuni ya Steps Int.

Ingia sokoni kupata nakala yako halisi kukuza sanaaa ya Tanzania.

WALTER: Talkin' After Ushindi


Chamillionaire: "I'm Comming"

Rapper Chamillionaire yupo tayari kurudi na Project Mpya ya Elevate. Fahamu kuwa Chamillionaire ameka kimya kwa miaka 5 Bila wimbo kwenye radio wala video.

Rapper huyu from Houston alitangaza project hii kwenye facebook page yake nakusema, FEB 12th on www.chamillionaire.com. The first 500 copies will be autographed and each autographed copy will be numbered…

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA