Jinsi ya kununua BUM KUBAM DVD ya NICK WA PILI Angalia hii video

Kabla ya kucheck hiyo video 

MFUMO RAFIK(CODE NAMBA) WA USAMBAZAJI MUZIK NA FILAMU TANZANIA

Ukitaka kununua bum kubam dvd ya nikk wa pili, Unaingia  Mpesa kwa kupiga *150*00# , kisha unachagua lipa bili yako kwa kuchagua namba 4, kisha unaweka namba ya kampuni yetu ambayo ni 212121, kisha unaweka kumbukumbu namba ya malipo ambayo ni jina la dvd ambayo ni Bum Kubam , kisha unaweka kiasi 4000, na kufata maelekezo. Baada ya malipo kukamilika,mda mchache baadaye utapokea meseji kutoka fichuka ambayo itakupa code namba ya hiyo dvd uliyonunua. 

  Baada ya kupata code namba utatakiwa kwenda kwa wakala wa fichuka aliye karibu nawe ambaye atahakiki code namba yako na kukupa DVD/CD , pia utapata maelekezo ya meseji ya njia rahisi ya kufahamu wakala wa karybu alipo. Kwa maana nyingine DVD/CD haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi.
FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
Ni mfumo rafiki kwa sababu ni mfumo unaopunguza vichocheo vya wizi wa kazi za wasanii kwa kufanya yafuatayo,

1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo huu ambapo atakua na akaunti yake ambapo ataweza kuona idadi ya nakala zote alizouza na mahali zilipouzwa.

2. Kwa sababu jamii itafahamu kwamba bidhaa hii haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi na anayefanya hivyo ni mwizi, itazuia wauzaji  wezi kuuuza bidhaa hii. Muuzaji anatakiwa ahakiki code namba sio kupokea  pesa.

3. Bidhaa yeyote inayonunuliwa kupitia mfumo huu ni lazima iwepo kwnye database yetu, kama unayo  bidhaa na haipo kwnye database yetu ni dhahiri kwamba umeshiriki katika kumuibia msanii na hatua za kisheria zitachukuliwa,

4. Msanii ana uwezo wa kufahamu kwa majina kila aliyenunua kazi yake na mda alionunua na anaweza pia kuwasiliana na wanunuzi kama atahitaji kufanya hivyo.

5. Kupitia mfumo huu, kazi ya msanii itakua inapatikana kiurahisi kama vocha dukani,  kwa hiyo itaongeza uhitaji wa kazi ya msanii na kupunguza mawazo ya kunakili kazi ya msanii.

6. Kwa kuwa wakala hanunui bidhaa, haingii gharama yoyote bali anapata commission itaongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji.

7. Kwa kuwa pesa anafaidika  moja kwa moja na mauzo ya kazi zake, wapenzi wa msanii watapenda kushiriki katika mfumo huu kwa kumsupport   msanii na kupata mawasiliano kutoka msanii moja kwa moja.

8. Kwa kuwa itakua inafahamika idadi ya nakala zote zilizouzwa itakua ni rahisi kucontrol soko la mzik na filamu Tanzania.

Bonyeza katikati kuAngalia jinsi ya kununua wimbo huo.......

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA