MILLARD-MIAKA YANGU 6 NYUMA

ALICHOANDIKA MILLARD AYO KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK LEO Ni moja kati ya post zisizo na picha lakini imepata LIKES, COMMENTS na SHARE nyingi kuliko zote alizowahi kuandika.

HIKI ndicho alichoandika..(MAISHA NA MAPENZI)

"Miaka 6 iliyopita wiki kama hii ndio nilipata tuzo ya kwanza ya Utangazaji kutoka Tanzania Radio Awards, nikapandishwa mshahara toka elfu tano mpaka elfu kumi kwa wiki kwenye radio niliyokua nikifanyia kazi, sikutamani kufanya kazi nyingine japo nilikua naishi kwenye hali ngumu sana, niliahidi nitapambana ili nifanikiwe kwa hii kazi kwa sababu naamini Mungu ameweka kitu ndani yangu, nasema Amen leo nina maisha ninayoridhika nayo kabisa tena sana, Namshukuru Mungu sana kwa hilo! hii ni maalum kwa watu wangu wote wa nguvu ambao wanapitia shida, hawana kazi au wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni, wanatafuta kazi kila siku hawapati, ukweli ni kwamba SUBIRA ni kila kitu, Nidhamu ni kila kitu, Maombi ni kila kitu, Kujituma ni kila kitu! kutokakuta tamaa ndio muhimu kabisa."
Millard akiinterview na Rosee..
Kila la kheri kaka ktk kazi zako..

SHILOLE&CHILLAH - DUDU Video

Official Video ya msanii SHILOLE feat. CHILLAH. Nyimbo inaitwa DUDU na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri Shabani.

RAY C AMSHUKURU KIKWETE KWA KUSAIDIA KUPONA KWAKE

Msanii wa kike wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amemshukuru sana rais kwa kumsaidia kupona kwake leo alipopata nafasi ya kumtembelea Ikulu.
 
Ray C ni moja kati ya watu waliokuwa waathirika wa madawa ya kulevya kupelekea afya zao kuwa mbaya..
Ray C kulia akiwa na Rais Kikwete.
Kutoka kushoto ni Bibi wa Ray C, Rais Kikwete, RayC na Dada yake.

R.I.P. MZEE ELEBUWA NOLLYWOOD

Mwigizaji nguli toka nchini Nigeria Enebeli Elebuwa (65) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini India kutoka na ugonjwa wa kupooza uliompata mwaka 2011.

Alianza kuigiza mwaka 1967 na alikuwa anavutia sana akiigiza kama mfalme au 'pedeshee' na filamu nyingi ameigiza hivo.


Hizi ni baadhi ya filamu alizowahi igiza Lost Kingdom, Abuja Connection, Sensational, Dons in Abuja, The Corridors of Power, Men Do Cry, Who Will Tell The President, and Royal War.

YOUR NEW MAISHA PLUS STAR

Bereniki Kimiro ndiye ametangazwa kuwa mshindi wa Maisha Plus kwa mwaka 2012 kwa kuwashinda wenzake.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Venance Kimaro na nafasi ya tatu imekwenda kwa Justine ambaye anatoka mkoani Dodoma.

Kila la Kheri bibie na hizo Mil. 20...

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA