Mbeya: BIBI MBARONI NA LITA 9 ZA GONGO ni muuzaji kitamboo



Mfano: Uandaaji wa Gongo
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia Bibi wa miaka 62, Marry Mbuya mkazi wa Kabwe jijini Mbeya kwa tuhuma za uuzaji wa pombe haramu  (Gongo).

Polisi wakiwa katika doria walimkamata mtuhumiwa nakiwa na lita 9 za pombe hiyo ya moshi jana asubuhi akiwa maeneo ya Mwanjelwa na jitihada za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha tukio hilo na kuwaasa watu kuachana na matutumizi ya pombe hiyo kwani ni kinyume na sheria pia hatari kwa afya zao.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA