Mbeya: AMUUA MWENZAKE KISA MWANAMKE WA KILABUNI


Pic: Mfano.

MKAZI  wa mtaa wa Itiji mkoani Mbeya, Daniel Mwasalemba, ameuawa kwa kuchomwa kisu na Peter Bosco wakigombania mwanamke wa kirabuni , Elizabeth Michael.

Ugomvi huo ulianza juzi wakiwa kirabuni na ukaamuliwa na wateja wengine ambapo Peter aliondoka na msichana huyo wa miaka 18 na kwenda nae nyumbani na kumpa kichapo ambapo alifanikiwa kutoroka na kurudi kilabuni ambapo alikutana na Daniel na baadae walirudi nyumbani pamoja .

Usiku wa kuamkia leo ndio Peter alirudi ktk hiyo nyumba na kuwa kuta kisha akwafungia mlango na kwenda kutafuta kisu a aliporudi akabomoa mlango na kumchoma kisu Daniel na kumsababishia kifo

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha tukio hilo na kuwa wameukuta mwili wa marehemu kando ya barabara ukiwa uchi (bila mavazi).

Jeshi la polisi linamshikilia Elizabeth kwa mahojiano kwani Peter amekimbia na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitalini.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA