Habari kutoka Washington zinasema kuwa watu 4 wameuawa na
wengine 8 kujeruhiwa baada ya mtu asiyejulikana kuvamia makao makuu ya jeshi la
wanamaji mjini Washington na kuanza kufyatua risasi.
Habari zaidi zinasema kuwa mtu huyo bado hajapatikana ingawa
inaaminika bado yuko katika jengo hilo.
Wakuu wa kituo hicho cha kijeshi wanasema maafisa kadhaa wamepigwa
risasi na mvamizi huyo.
Polisi zaidi wamepelekwa kwenye eneo hilo huku shughuli
katika uwanja wa ndege wa Reagan ulioko karibu zikisitishwa kwa muda.
Zaidi ya wafanyakazi 3000 wanafanya kazi katika kituo hicho
kilichovamiwa. Kitengo hicho kijulikanacho kama Naval Sea Systems Command
ndicho kinachohusika na utengenezaji, ukarabati au ununuzi wa meli za kijeshi
pamoja na nyambizi za jeshi la Marekani.
Haijabainika ni vipi mtu huyo aliweza kuingia katika eneo
hilo lenye ulinzi mkali.
No comments:
Post a Comment