InfoGramme: FAMILIA WAMEKUFA KWA MOTO MBEYA

WAKAZI wa Ilemi, jijini Mbeya mkoani hapa, Fadhir Said na mke wake, Lucy Said, wamefariki dunia baada ya kuungua na moto baada ya nyumba yao kushika moto na kuwaka usiku wa kuamkia leo.

Fadhir na mkewe, wameungua na moto huo wakiwa katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yao hiyo iliyopo maeneo ya Ilemi. Wakiongea na InfoGramme, majirani wa familia hiyo, wameeleza kuwa moto huo ulizuka mida ya saa 6 za usiku wakiwa wamelala na kusaidiana kuuzima.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi wa Polisi, Diwani Athumani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Kamanda Athumani amesema kuwa, hakuna mtu yeyote zaidi aliyedhurika na moto huo, ingawa marehemu hao walikuwa wanaishi na familia yao yenye watoto wanne.
Thamani ya mali zilizoharibika haijafahamika na iili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA