Check Story ya Mtangazaji anayedai kupigwa risasi 2nduma


Mwandishi wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma, katika wilaya mpya ya Momba mkoani hapa,  Shomi Mtaki, amepigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi shambani kwake.
Ikiwa ni kipindi kifupi baada ya taaarifa za mwandishi wa ITV, Ufoo Saro, kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Mtaki alivamiwa na watu 5 waliokuwa na siraha.
Watu hao waliokuwa na bunduki walimlazimisha Mtaki kutoa fedha alizokuwa nazo baada ya kuvunja mlango wa nyumba alimokuwamo kwa jiwe kubwa.

Bada ya wavamizi hao kutoweza kuvunja mlango kwa jiwe, walianza kumimina risasi kwenye mlango hua ambapo ilimpata moja mguuni.
Mtaki amesema kuwa yeye na mkewe walijaribu kujiokoa maisha yao ambapo mkewe aada ya kusikia mlio wa risasi aliingia chini ya mvungu wa kitanda.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, amekiri kutokea kwa tukio hilo la uvamizi na kusema kuwa jeshi la polisi liaendelea na uchunguzi. 

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA