Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa zaidi ya asilimia
12 ya jamii ya watu duniani, wanakabiliwa na njaa.
Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika hilo, Jose Silva, ameeleza kuwa, kutokana na wastani huo, ina maana
kwamba mtu mmoja kati yawatu 8 ana tatizo la ukosefu wa chakula.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa, watu milioni 840 wanakabiliwa na ukosefu wa
chakula kwa mwaka huu ambapo idadi hiyo imepungua kutoka watu milioni 870 kwa
mwaka jana.
No comments:
Post a Comment