BOKO HARAMU WAUA WENGINE 19, BAADA YA 80 WA JUZI

WATU 19 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno nchini Nigeria, kwenye kizuizi cha barabarani walichokuwa wameweka.
 
Wanamgambo hao, wamewaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kuwanyonga wengine 14 na baadae walitokomea baada ya kupata taarifa za wanausalama kuja eneo la tukio.
 
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, Wanamgambo hao waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, waliweka kizuizi barabarani na kuanza kuwapiga risasi madereva.
 
Katika tukio jingine, wapiganaji hao wa Boko Haram wamewaua watu 87 kwenye shambulio katika Jimbo la hilohilo nchini Nigeria.
 
Mashahidi wanasema kuwa wapiganaji hao wameteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA