Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya
mwigizaji Lulu iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na
kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam,
kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja
na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za
kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti
yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la
msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa
ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu
kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi
wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia
saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.
Mama mzazi wa Lulu akiwa mahakamani kusikiliza Dhamana ya mwanaye. (Wa 2 kutoka kushoto)
Lulu akibembelezwa kupigwa picha na mwandishi mmoja wa kike
Lulu akisikiliza Dhamana yake na Masharti aliyopewa.. PICHA zote na MillardAyo.Com
Jana kwenye Exclusive on
millardayo.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu
kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.
Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa zilizotolewa kwa Millard Ayo ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.
Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.
Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa
katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate
dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani)
ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.
Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.
Taarifa za uhakika nilizozipata
kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana
kesho Tarehe 25.
Uhakika wa Lulu kupata dhamana
ulikua jana jumatano lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa
sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua
hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika kimesema
dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni
milioni 20 za kitanzania.
Lulu amekua akishikiliwa kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba tangu April 2012, endelea
kuipitia abrangula.com kwa stori zaidi.
Ile picha iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha Diamond anajipaka poda ndani ya gari akiwa na msichana basi Script yake ilikuwa ya humu ndani, tizama video mpya ya Keisha akiwa na Diamonda track inaitwa nimechoka kupitia InfoGramme Blog.
Kuhusu Video hii Keysha amesema, "Nimetumia zaidi ya shilingi za Tanzania Milioni 10 kuandaa video hii,
hii ikiwa ni pamoja na malipo kwa AJ ambaye amesimamia kazi yote, video
hii ilikuwa itoke muda mrefu lakini kutokana na msururu wa ratiba ya
shoo za nje ya nchi nilijikuta mara kadhaa ninahirisha kushoot,
nashukuru Mungu imekamilika na huu ni mwanzo wa mafanikio yangu katika
mwaka huu wa 2013"
Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Qubanda a.k.a
Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye
ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma "Under The Same Sun" kwa mchango wake
mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Fid Q amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa
shirika hilo la Canada, Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi
yanayosomeka.. "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and
only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."
Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa
kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu
kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.
Jiandae kuwa Mmoja ya watakaotumia Vyema
Dakika 90 Bora., Mbeya FM inakupa nafasi ya kutumia Dakika 90 Bora kwa
Usafiri bora na wa Uhakika wa Anga kwa kutumia Precision
Air..!!#Tafadhali sikiliza 89.5 Mhz Mbeya FM muda wote uwe moja ya
Washindi.#Team-Mbeya FM#
Mtoto
katoka shuleni huku analia, alipofika nyumbani. Baba yake akamuuliza
''unalia nini'? MTOTO '' Nimepigwa na mwalimu na nimeambiwa twende wote
shuleni''. Wakaenda shuleni na wakaingia ofisini. MWALIMU ''Karibuni,
mtoto wako tumemuuliza Nairobi iko wapi kashindwa, ndio maana
tumemchapa'' Baba akamgeukia mtoto wake na kumpiga vibao, akamwambia
''mpumbavu mkubwa, kila siku nakukataza kuchezea vitu vya watu hukomi,
haya NAIROBI ya mwalimu umepeleka wapi'?
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia Bibi wa miaka 62,
Marry Mbuya mkazi wa Kabwe jijini Mbeya kwa tuhuma za uuzaji wa pombe
haramu(Gongo).
Polisi wakiwa katika doria walimkamata mtuhumiwa nakiwa na
lita 9 za pombe hiyo ya moshi jana asubuhi akiwa maeneo ya Mwanjelwa na
jitihada za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha
tukio hilo na kuwaasa watu kuachana na matutumizi ya pombe hiyo kwani ni
kinyume na sheria pia hatari kwa afya zao.
Huu ndio uzinduzi wa track ya Izzo B aliyomshirikisha QuickRocka na Mangwair iitwayo Ball Player ambayo imeachiwa rasmi Jumatano ya leo.. Fuata link hii kuiskiliza na kudownload.. Bofya HAPA (By Infogramme Blog)
Hemedy Suleiman baada ya kuachia ngoma yake mpya mwaka jana inayokwenda kwa jina la Going Crazy kutoka B hits alisema anatarajia kuachia video yake siku ya Valentine day lakini leo ipo hewani. Tizama Video hiyo kwa kubofya hapo katikati..
Izzo B amesema kuwa Juma tano hii anaachia ngoma yake ya kwanza kwa mwaka 2013 iitwayo Ball Player ambayo amemshirikisha Mangwair na Quick Rocka, Ngoma hiyo imetengenezwa na Nahreel na Lamar.
Cover ya track hiyo iliyotupiwa na Ngwair ktk Twitter
MFUMO RAFIK(CODE NAMBA) WA USAMBAZAJI MUZIK NA FILAMU TANZANIA
Ukitaka kununua bum kubam dvd ya nikk wa pili, Unaingia Mpesa kwa kupiga *150*00# , kisha unachagua lipa bili yako kwa kuchagua namba 4, kisha unaweka namba ya kampuni yetu ambayo ni 212121, kisha unaweka kumbukumbu namba ya malipo ambayo ni jina la dvd ambayo ni Bum Kubam , kisha unaweka kiasi 4000, na kufata maelekezo. Baada ya malipo kukamilika,mda mchache baadaye utapokea meseji kutoka fichuka ambayo itakupa code namba ya hiyo dvd uliyonunua.
Baada ya kupata code namba utatakiwa kwenda kwa wakala wa fichuka aliye karibu nawe ambaye atahakiki code namba yako na kukupa DVD/CD , pia utapata maelekezo ya meseji ya njia rahisi ya kufahamu wakala wa karybu alipo. Kwa maana nyingine DVD/CD haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi. FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
Ni mfumo rafiki kwa sababu ni mfumo unaopunguza vichocheo vya wizi wa kazi za wasanii kwa kufanya yafuatayo,
1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo huu ambapo atakua na akaunti yake ambapo ataweza kuona idadi ya nakala zote alizouza na mahali zilipouzwa.
2. Kwa sababu jamii itafahamu kwamba bidhaa hii haiuzwi kwa kupokea pesa mkononi na anayefanya hivyo ni mwizi, itazuia wauzaji wezi kuuuza bidhaa hii. Muuzaji anatakiwa ahakiki code namba sio kupokea pesa.
3. Bidhaa yeyote inayonunuliwa kupitia mfumo huu ni lazima iwepo kwnye database yetu, kama unayo bidhaa na haipo kwnye database yetu ni dhahiri kwamba umeshiriki katika kumuibia msanii na hatua za kisheria zitachukuliwa,
4. Msanii ana uwezo wa kufahamu kwa majina kila aliyenunua kazi yake na mda alionunua na anaweza pia kuwasiliana na wanunuzi kama atahitaji kufanya hivyo.
5. Kupitia mfumo huu, kazi ya msanii itakua inapatikana kiurahisi kama vocha dukani, kwa hiyo itaongeza uhitaji wa kazi ya msanii na kupunguza mawazo ya kunakili kazi ya msanii.
6. Kwa kuwa wakala hanunui bidhaa, haingii gharama yoyote bali anapata commission itaongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji.
7. Kwa kuwa pesa anafaidika moja kwa moja na mauzo ya kazi zake, wapenzi wa msanii watapenda kushiriki katika mfumo huu kwa kumsupport msanii na kupata mawasiliano kutoka msanii moja kwa moja.
8. Kwa kuwa itakua inafahamika idadi ya nakala zote zilizouzwa itakua ni rahisi kucontrol soko la mzik na filamu Tanzania.
Bonyeza katikati kuAngalia jinsi ya kununua wimbo huo.......
Mtu asiyefahamika aliibuka jukwaani na kumnyooshea bastora mwanasiasa Ahmed Dogan wa nchini Bulgaria na kutaka kumuua kwa kumuelekezea kichwani na baadae ukatokea mkanganyiko na kushindwa kufanikiwa. Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Angalia video hii ujionee.....
Shukrani za pekee zije kwako wewe unayeendelea kutembelea www.infogramme.blogspot.com na kusupport muziki wa Mbeya na kizazi kipya kwa namna moja ama Nyingine.. Kwa niaba ya wadao wa mziki Mkoa wa Mbeya nasema ASANTEE!!
Filamu aliyoigiza Marehemu Sajuki na mkewe Wastara iitwayo KIVULI imeingia sokoni rasmi leo. Filamu hiyo imeandaliwa na kampuni yao Wajay Film Co. na kusambazwa na kampuni ya Steps Int.
Ingia sokoni kupata nakala yako halisi kukuza sanaaa ya Tanzania.
Rapper Chamillionaire yupo tayari
kurudi na Project Mpya ya Elevate. Fahamu kuwa Chamillionaire ameka kimya kwa
miaka 5 Bila wimbo kwenye radio wala video.
Rapper huyu
from Houston alitangaza project hii kwenye facebook page yake nakusema, FEB
12th on www.chamillionaire.com. The first 500 copies will be autographed and
each autographed copy will be numbered…