AmmyChiba: Mpe Support huyu dada wa Green City kwenye EBSS. Hapa ni VIDEOZ: Track yake na wakati akiongea na Infogramme Blog

VIDEO: UTAMU wa Epiq Bongo Star Search umeanza

Jumapili hii ndani ya Club BILLZ 'Chid B'


BIFU YAISHA: Man Walter na 20% Beef BASI


Kwenye ukurasa wa facebook wa Magic Fm na Channel Ten taarifa hii imetolewa hivi..
Hatimaye bifu kali kati ya msanii aliyewahi kutwaa tuzo 5 za KTMA nchini kwa pamoja na kuvunja rekodi, TWENTY PERCENT na aliyewahi kuwa Producer wake pia mshindi wa tuzo ya matayarishaji bora wa muziki nchini KTMA 2012, MAN WATER, limemalizika rasmi  kwa wawili hao kukutana na kumaliza tofauti zao. 
Man Water na Twenty Percent walikutana na wawili hao wamekubaliana kufanya kazi tena pamoja na kusahau yaliyopita.
Akizungumzia kiundani kuhusu tofauti zao Man Water alisema tatizo lilikua ni kutoelewana au kupishana kwa kauli ambazo walizimaliza na hatimaye kuweka mikakati mipya ikiwemo ya kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalumu.
Kwa upande wake 20% amesema tofauti zao hazikuwa za msingi bali ni kupishana tu kwa kauli na sasa yuko tayari kufanya kazi pamoja na Man Water.
Inaaminika kwamba kufanya kazi pamoja kwa wawili hao kunaleta mwamko mkubwa kwa washabiki wao kutokana na kuelewana katika kazi zao mbalimbali walizowahi kufanya ikiwemo kaziya Yanini malumbano, Tamaambaya, Mama Neema na nyinginezo.

Kutana na msumbufu Yohana Charles..!

AU kujadili hoja ya kujiondoa ICC


Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini Addis Ababa Ethiopia, kujadili msimamo wa bara hili kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifiu - ICC.
Mkutano huo unafuatia ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kujadili kesi zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Kwa sasa hakuna dalili kuwa kuna msimamo mmoja kuhusu ikiwa wanachama 54 wa Muungano wa Afrika waliotia saini mkataba wa Roma wanataka kujiondoa, lakini marais wa nchi hizo bado watajadili uwezekano wa wanachama 34 wa mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC watajiondoa ICC.Mwandishi wa BBC mjini Addis Aabab, Emmanuel Igunza anasema kuna dalili kuwa ombi hilo la Kenya limeanza kuungwa mkono na mataifa mengi barani.
Tangu kuanza kwa kesi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC wiki jana, na ile ya Rais Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Novemba, dalili zimeonekana kuwa wengi hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi kukandamiza waafrika.
Kikao cha dharura sasa kimepangwa kujadili swala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka kuungwa mkono katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna uwezekano wa nchi wanacahama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna nafasi ya maombi mengine kufanywa kuhusiana na hilo.

ICC yataka mwandishi wa Kenya akamatwe

Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa raia Mkenya ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kuwahonga mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Viongozi wa mashtaka walisema kuwa mshukiwa huyo Walter Osapiri Barasa ameshtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kutumia njia za ufisadi kumshawishi shahidi mmoja na mkewe kwa kumlipa shilingi milioni 1.4 au dola 16,200, ili wajiondoe kama mashahidi katika kesi hiyo.
Aidha mahakama inasema kuwa ni juu ya Kenya sasa kumkamata Barasa..

Skiliza na Download Mixing kali za Dj Speed 4rm Hylands FM Mby, So Crazzzy

Pics: Check out Kilivyonuka Mwanjelwa Mbeya


Wishes: Happy Birthday DIAMOND PLATNAMZ

Katika ukurasa wake wa FaceBook Diamond ameandika "HAPPY BIRTHDAY MIMI"

NU Audio: East U "VITA MADAWA" GreenCity UP

BONGE LA HIT: Chanty Bizzy - "GHETTO PARADISE" Audio.. Iskize na Download hapa...

TAARIFA: LIGI daraja la 4 mjini Mbeya kuanza soon


Ligi ya daraja la nne jijini Mbeya inategemea kuanza hivi karibuni endapo zoezi la kurudisha na kupokea fomu likamilika siku ya leo.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu jijini Mbeya, Watson Mwakisole, amesema kuwa ligi hiyo inatarajia kuanza tarehe 21 mwezi huu baada ya taratibu za awali kukamilika. Amezitaja timu 14 zinazotarajia kushiriki ligi hiyo ikiwa ni pamopja na timu ya Prison Junior ambayo ni timu mwalikwa.

Mwakisole ameeleza kuwa Prison Junior itashiriki ligi hiyo na endapo ikipata ubingwa itapewa zawadi isipokuwa hawatocheza ligi ya mkoa kwani hii ni kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya uhai.

Katibu huyo ameongeza kwa kueleza changamoto wanayokutana nayo kuwa ni kutokuwa na wadhamini wa ligi hiyo.

NGASSA ALIVYOWASILISHA MILIONI 45 ZA SIMBA TFF JIONI HII

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (katikati) akiwa ameshika risiti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kulipa Sh. Milioni 45, alizotakiwa kuilipia klabu ya Simba SC. Wengine kulia ni Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto na kushoto Mhasibu, Rose Msamila. Ngassa alifungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na kutakiwa kurejesha fedha za Simba Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, baada ya kubainika alisai timu mbili, Simba na Yanga alikoidhinishwa kucheza msimu huu..

EMPIRE CHANT BIZZY & NYANDSON - REVOLUTION (OFFICIAL VIDEO)


Kenya yaapa kumsaka Samantha Lewthwaite

Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.

MSANII WA KIZAZI KIPYA MIEZI 6 JELA KWA WIMBO WA MATUSI

Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.

Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.

Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa.

MCHINA ametengeneza pua mpya katika paji la uso baada ya ajali iliyoharibu poa yake



Raia mmoja wa china, Xiaolian mwenye miaka 22 amefanyiwa matibabu ya kutengeneza pua mpya ambayo itachukua nafasi ya pua yake ambayo ilipata madhara alipopata ajali ya barabarani.


Xiaolian Ameoteshwa pua kwenye paji la uso wake baada ya wataalam kushindwa kuiponya ile iliyoharibika baada ya ajali.


Utengenezaji wa pua hiyo mpya, umefanywa kwa kuchukua sehemu ya mbavu za binadamu kwa kukatwa kwa muundo wa pua.


Madaktari wamesema mwanaume huyo anaendelea vizuri na zoezi la kuipandikiza pua hiyo mpya eneo la pua ya zamani utafanyika hivi karibuni.

WALOKUFA KENYA WAFIKIA 68, WAMAREKANI WAHUSIKA KUSHAMBULIA, Mateka wanaendelea kuokolewa

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Kenya kutokana na shambulio la ugaidi la Al Shabab imeongezeka na kufikia 68, na uokoaji unaendelea vizuri. Kundi la Alshabab limedai kuwa miongoni mwa wafuasi wakewalioteketeza shambulio hio watatu ni raiawa Kimarekani, FBI wachunguza.

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA