HEMEDI: Video ValentineDay

Hemed Suleiman baada ya kuachia ngoma yake mpya mwaka jana inayokwenda kwa jina la Going Crazy kutoka B hits, sasa basi anatarajia rasmi kuachia video yake mpya siku ya tarehe 14 Valentine Day.Kaa tayari kwa ujio huu mpya kutoka kwa PHD.

COMING SOON: FA - The Finest



Kama wewe ni shabiki wa Mwana FA basi huu ndiyo ujio wake mpya 2013 ambao anatarajia kuuachia siku za hivi karibuni kaa tayari kwa ujio kutoka kwa msanii huyu.

HUU NDIO WIMBO WA WABABA MTUKA, NO 3 EBSS 2012

Wababa Mtuka mshiriki na mshindi wa tatu wa Epiq BSS 2012

INTRO:                                                  
Ema the boy mmh! mmh!
VERSE  1
 Kiukweli sina hata la kusema my wife
Ajali nyingi za mapenzi nilopata unajuaaa  

ooh! unajuaa ! machozi niliyoliaa!
Usiku na mchana usibhabhakulunjalibhan
Baby usije kata tamaaa Vulu vulu vulu!

 CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

VERSE 2.
Iye he!  Kama mapenzi ni kung'ang'ana { Basi ng'ang'ana 

Na kama mapenzi unajua sana { Basi kazana
Mukikiki, nasijawahi,mapenzi yako sioni tena
Omwanajhonteme,nakupenda Habibi uhibuk { Nakuwaza}
Naweza wa hatakwanaino { Hata kwanaino}
Halikosi na mikingamo { Nami kingamo}
 Nawahi wahi,watusome,pia wajue,wanipa raha
Ninachotaka,jitulize,jiwekebize, hapontafurahiiii
Ey Vulu vulu vulu.

CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

VERSE 3.
Iye he!  Zito haliwi zito kwanza mpaka lipimwe

Tabia ya mtu ni kama ngozi ukiweza fasta ivue
Nai na nai nai nai nai x2
Ukiona nyani porini najiweka Ujue na ficha mkia wangu
{ Nai na nai nai nai nai }x2
Mh uko fitifiti kwa kitikiti, Unahitihiti, kwa mutimuti
Yani huchoshi choshi, Sikoshikoshi
Nikilala shishishi,Unatishitishiii Eeeh aaaaah

CHORUS
I say you are my wife                        {i say  my wife}
Ukiniacha ntaliaaa                            {i say  my wife}
you are my my my wife  aaai            {i say  my wife}
Lele lele my my my wife Eeeh!          {i say  my wife}

KUHUSU DIAMOND NA WOLPER



Diamond Amekanusha Uvumi kuwa anamahusiano ya Kimapenzi na Jaqueline Wolper Nakusema Kuwa Picha zilizo onyweshwa kwenye magazeti ni za video ya Keisha 'Nimechoka' aliyo Shirikishwa Diamond. Plantnumz amesema video shoot ya wimbo huu ilianza Miezi miwili iliyopita na kuja kukamilika wiki Mbili zilizo pita na ndio scene ya video hio inamuonyesha akiwa karibu na Wolper.
Hiki ndicho kilichoandikwa Gazetini..
Pia Diamond amesema Msichana yoyote atakaye sema ni Girl Friend wake kwa sasa Ni Muongo kwani yeye yupo single kwa sasa na hana mpango wa kutangaza Mpenzi wake atakaye mpata. Diamond Alikaririwa na sammisago.com akisema `Simba akiwa Karibu na Swala, Watu wanadhani Anamla, Ila Kuna Muda Simba Anashiba'

Darasa Ft.Winnie - NishikeMkono(Official Video)


MILLARD-MIAKA YANGU 6 NYUMA

ALICHOANDIKA MILLARD AYO KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK LEO Ni moja kati ya post zisizo na picha lakini imepata LIKES, COMMENTS na SHARE nyingi kuliko zote alizowahi kuandika.

HIKI ndicho alichoandika..(MAISHA NA MAPENZI)

"Miaka 6 iliyopita wiki kama hii ndio nilipata tuzo ya kwanza ya Utangazaji kutoka Tanzania Radio Awards, nikapandishwa mshahara toka elfu tano mpaka elfu kumi kwa wiki kwenye radio niliyokua nikifanyia kazi, sikutamani kufanya kazi nyingine japo nilikua naishi kwenye hali ngumu sana, niliahidi nitapambana ili nifanikiwe kwa hii kazi kwa sababu naamini Mungu ameweka kitu ndani yangu, nasema Amen leo nina maisha ninayoridhika nayo kabisa tena sana, Namshukuru Mungu sana kwa hilo! hii ni maalum kwa watu wangu wote wa nguvu ambao wanapitia shida, hawana kazi au wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni, wanatafuta kazi kila siku hawapati, ukweli ni kwamba SUBIRA ni kila kitu, Nidhamu ni kila kitu, Maombi ni kila kitu, Kujituma ni kila kitu! kutokakuta tamaa ndio muhimu kabisa."
Millard akiinterview na Rosee..
Kila la kheri kaka ktk kazi zako..

SHILOLE&CHILLAH - DUDU Video

Official Video ya msanii SHILOLE feat. CHILLAH. Nyimbo inaitwa DUDU na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri Shabani.

RAY C AMSHUKURU KIKWETE KWA KUSAIDIA KUPONA KWAKE

Msanii wa kike wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amemshukuru sana rais kwa kumsaidia kupona kwake leo alipopata nafasi ya kumtembelea Ikulu.
 
Ray C ni moja kati ya watu waliokuwa waathirika wa madawa ya kulevya kupelekea afya zao kuwa mbaya..
Ray C kulia akiwa na Rais Kikwete.
Kutoka kushoto ni Bibi wa Ray C, Rais Kikwete, RayC na Dada yake.

R.I.P. MZEE ELEBUWA NOLLYWOOD

Mwigizaji nguli toka nchini Nigeria Enebeli Elebuwa (65) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini India kutoka na ugonjwa wa kupooza uliompata mwaka 2011.

Alianza kuigiza mwaka 1967 na alikuwa anavutia sana akiigiza kama mfalme au 'pedeshee' na filamu nyingi ameigiza hivo.


Hizi ni baadhi ya filamu alizowahi igiza Lost Kingdom, Abuja Connection, Sensational, Dons in Abuja, The Corridors of Power, Men Do Cry, Who Will Tell The President, and Royal War.

YOUR NEW MAISHA PLUS STAR

Bereniki Kimiro ndiye ametangazwa kuwa mshindi wa Maisha Plus kwa mwaka 2012 kwa kuwashinda wenzake.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Venance Kimaro na nafasi ya tatu imekwenda kwa Justine ambaye anatoka mkoani Dodoma.

Kila la Kheri bibie na hizo Mil. 20...

ALICHOANDIKA WALTER KTK BLOG YAKE YA chilambo.blogspot.com

NAOMBA niwaahidi mashabiki wangu kuwa hivi karibuni kama MUNGU  akipenda ndani ya hizi wiki mbili (2) nitaachia ngoma yangu mpya ya kwanza Officially na naamini kama itakuwa poa kwa jitihada zangu katika hilo

Nitatoa maelezo yote ya nyimbo hiyo hapahapa kabla hata ya kuitoa kama nimetengeneza wapi na Producer gani na jua kuwa utakuwa utunzi wangu mimi mwenyewe.
Pia kuhusiana na Collabo yangu na Ben Pol, Hata kabla Ben Pol kusema kuwa anataka Collabo na mimi, Yeye ni moja kati ya wasanii ninao wakubali na ndio maana hata wimbo wake ulikuwepo katika listi ya nyimbo zangu nilizoimba FINALE.
Ben Pol akimtuza Walter siku ya FINALE
Hivyo kwa sasa naona ndoto zangu zinatimia, hivyo watu wangu wategemee ngoma yangu na Ben Pol kwani kilichobaki ni kuongea nae na kufanya kazi tuu,Jua kuwa NIKIKUPATA ya BEN POL  ni wimbo ulonifanya kuwa STAR kuliko nilivyofikilia.
Nawapenda sana watu wangu na nawaomba tuendelee kuwa pamoja katika kazi zangu kwani jua kabisa kuwa hakuna MIMI bila WEWE.

CHEKA NA ABBY

Zuzu mmoja alipita sehemu flani akakuta
watoto wanacheza, akawadangaya wale
watoto,
"Nyie nendeni kule kuna chakula
kinagawanywa." Wale watoto kuskia hivyo wakatimua
mbiooo! Zuzu kuona watoto wametoka mbio
akajisemea moyoni,"Mbona wanakimbia
mbio sana labda kuna chakula kweli." Naye akaanza kukimbia ili kuhakikisha kama
kipo kweli.....

MTOTO MIAKA 5 AGONGWA NA KUFA.

Na Abbin Nelson, Mbeya.
Mtoto wa miaka mitano, Peresi Antony, amegongwa na gari na kufa papo hapo katika maeneo ya kijiji cha Shamengo wilaya ya Mbeya vijijini kutokana na mwendokasi wa dareva, Mini Mussa (36) ambaye amekamatwa na yupo chini ya ulinzi wa polisi kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.
Mashuhuda ambao ni majirani na maeneo ambapo ajalio imetokea walisema kuwa dereva huyo alikuwa katika mwendo mkali sana kiasi kwamba hata ajali ilivyotokea huwezi kusema kuwa ni kwa bahati mbaya.
Mwili wa marehemu mtoto Peresi umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoani hapa kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi amethibitishakutokea kwa tukio hilo na kuwaonya madereva kutoendesha magari kwa mwendo mkali hata kama sio magari ya abiria.

LALA PEMA PEPONI BABA

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanzania toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985. Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Maisha yake Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 ( katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania). Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika. Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. 05.02.1977 aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake. Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi raisi wa pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamini W.Mkapa kama mgombea wa raisi wa mwaka 1995 na ambaye aliteuliwa kuwa raisi kwenye uchaguzi wa mwaka 1995. Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Tar. 14.10.1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas London baada ya kupambana na kansa ya damu. Mafanikio (kujenga umoja wa Taifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitani dhidi Idi Amin) Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo) Kutofanikiwa Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya uraisi baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani kwa Ali Hassan Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria. Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumwaga juu ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.” Ukosoaji dhidi yake Nyerere analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Pia kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa wakristo. Sifa zake Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu. Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24. Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama. Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere. • Freedom and Socialism.Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968) • Freedom & Development, Uhuru Na Maendeleo (1974) • Ujamaa - Essays on Socialism' (1977) • Crusade for Liberation (1979) • Julius Kaisari.Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius Caesar

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA