MTOTO MIAKA 5 AGONGWA NA KUFA.

Na Abbin Nelson, Mbeya.
Mtoto wa miaka mitano, Peresi Antony, amegongwa na gari na kufa papo hapo katika maeneo ya kijiji cha Shamengo wilaya ya Mbeya vijijini kutokana na mwendokasi wa dareva, Mini Mussa (36) ambaye amekamatwa na yupo chini ya ulinzi wa polisi kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.
Mashuhuda ambao ni majirani na maeneo ambapo ajalio imetokea walisema kuwa dereva huyo alikuwa katika mwendo mkali sana kiasi kwamba hata ajali ilivyotokea huwezi kusema kuwa ni kwa bahati mbaya.
Mwili wa marehemu mtoto Peresi umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoani hapa kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi amethibitishakutokea kwa tukio hilo na kuwaonya madereva kutoendesha magari kwa mwendo mkali hata kama sio magari ya abiria.

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA