NGASSA ALIVYOWASILISHA MILIONI 45 ZA SIMBA TFF JIONI HII
Mshambuliaji
wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (katikati) akiwa ameshika risiti ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kulipa Sh. Milioni 45,
alizotakiwa kuilipia klabu ya Simba SC. Wengine kulia ni Ofisa Habari wa
Yanga SC, Baraka Kizuguto na kushoto Mhasibu, Rose Msamila. Ngassa
alifungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na kutakiwa kurejesha
fedha za Simba Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, baada ya kubainika alisai timu mbili, Simba na Yanga alikoidhinishwa kucheza msimu huu..
Kenya yaapa kumsaka Samantha Lewthwaite
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke
aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia
Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana
duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
MSANII WA KIZAZI KIPYA MIEZI 6 JELA KWA WIMBO WA MATUSI
Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben
Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela
kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.
Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa
baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya
kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.
Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa.
MCHINA ametengeneza pua mpya katika paji la uso baada ya ajali iliyoharibu poa yake
Raia mmoja wa china, Xiaolian mwenye miaka 22 amefanyiwa matibabu ya kutengeneza pua
mpya ambayo itachukua nafasi ya pua yake ambayo ilipata madhara alipopata ajali
ya barabarani.
Xiaolian Ameoteshwa pua kwenye paji la uso wake
baada ya wataalam kushindwa kuiponya ile iliyoharibika baada ya ajali.
Utengenezaji wa pua hiyo mpya, umefanywa kwa kuchukua sehemu
ya mbavu za binadamu kwa kukatwa kwa muundo wa pua.
Madaktari wamesema mwanaume huyo anaendelea vizuri na zoezi
la kuipandikiza pua hiyo mpya eneo la pua ya zamani utafanyika hivi karibuni.
WALICHOANDIKA MAN U ktk ukurasa wa FaceBook Baada ya kipigo cha 4 - 1 na Man City
FT: City 4 United 1
Manchester City claim derby bragging rights, as the Blues run out convincing 4-1 winners at the Etihad Stadium.
Wayne Rooney netted a spectacular late winner with a long-range free-kick, but it was too little too late for the Reds, who had already conceded four times.
Manchester City claim derby bragging rights, as the Blues run out convincing 4-1 winners at the Etihad Stadium.
Wayne Rooney netted a spectacular late winner with a long-range free-kick, but it was too little too late for the Reds, who had already conceded four times.
Wliokufa KENYA Idadi imefikia 59, 175 Majeruhi
Video: SHAMBULIO LA KENYA. Vifo 39, 150 Wajeruhiwa
Raisi Uhuru Kenyatta athibitisha vifo 39 na wengine zaidi ya 150
kujeruhiwa na waliofanya shambulio ni Al Shabab.
PICHA&Maelezo: SHAMBULIO LA KENYA. Vifo 39 vyathibitishwa, Al shabab wakiri kufanya shambulio, 150 Wajeruhiwa
Afisa mkuu wa Alshabaab,
amefahamisha jamii kwa Twitter kuwa kundi hilo ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya
duka la kifahari la Westage mjini Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa Afisa huyo mashambulizi hayo
yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na vita vya
Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.
Raisi Uhuru Kenyatta athibitisha vifo 39 na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa na ameongeza kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na majeraha yake.
Dayna Nyange amekwangua ngozi ya mwili wake na kuwa Mweupeee
Wabunge wa Nigeria wapigana bungeni, Chama tawala cha PDP kimekuwa kikikumbwa na mgogoro wa ndani kwa muda sasa
Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana
ngumi wakati wa vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu
kuhusu mrengo wa wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni
kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni,
pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa
kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume
akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake.
Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya mwenyekiti
wa mrengo wa wabunge waliojiondoa kutoka kwa chama tawala, Kawu Baraje,
kuingia bungeni akiandamana na magavana wanaomuunga mkono.
Inaarifiwa spika wa bunge la waakilishi ,Aminu
Tambuwal, aliambia wabunge kuwa Baraje aliomba ruhusa kuwahutubia
wabunge wa mrengo wake kabla ya bunge kuanza vikao vyake.
Lakini kuwepo kwa wabunge hao bungeni
kuliwaghabisha mno wafuasi wa chama tawala, PDP,kiasi cha kuzuka
sokomoko bungeni kati ya pande hizo mbili na kumlazimisha bwana Baraje
kukatiza hotuba yake kutokana na kelele bungeni.
Chama tawala PDP kina wabunge wengi zaidi bungeni wakiwa 23 kati ya wabunge wote 36
Aidha chama hicho kimetawala Nigeria tangu
kupata uhuru mwaka 1999 lakini hivi kribuni kimezongwa na migogoro ya
ndani ya chama pamoja na kukabiliwa na upizani wenye ushawishi.
Wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mwaka 2015,
lakini wadadisi wana wasiwai ikiwa chama tawala kitakuwa kimesuluhisha
migogoro yake, huku kikikabiliwa na upinzani mkali.
Mgogoro huu umekuwa ukitokota kwa miezi kadhaa
huku baadhi ya wabunge wakitofautiana kuhusu ikiwa Rais Goodluck
Jonathan aidhinishwe na chama kugombea urais kwa mara nyingine wakati
kuna wanasiasa wengine wanaotaka kugombea urais.
Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa Nigeria kurushiana ngumi bungeni.
Kutoka Polisi Mbeya: MAKALA YA ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MICHEZO MKOA WA MBEYA
Katika maisha ya kila siku ya binadamu suala la ulinzi na usalama wa mali na maisha ni muhimu sana.
Binadamu huishi
kwa kutegemeana basi ndivyo ilivyo hata katika suala la ulinzi wa mali na
maisha yetu. Unaweza kujiuliza je,ni nani mwenye jukumu la ulinzi?je,ni mimi au
wewe? Au ni sisi sote?
Basi katika
miaka ya hivi karibuni Jeshi la Polisi Nchini limeendeleza dhana ya ulinzi
shirikishi na ulinzi jirani kwa lengo la kushirikisha jamii kwa karibu zaidi
katika suala zima la ulinzi na usalama. Zana hii imekuwa ikitoa fursa kwa jamii
na wadau mbalimbali kutoa taarifa za kuzuia uharifu hali inayofanikisha
kudhibiti vitendo hivyo.
Ni wazi
kabisa kuwa kila mmoja wetu ana jukumu la kushiriki katika ulinzi.Ushirikishwaji
huu wa wananchi katika kuzuia na kudhibiti vitendo vya uharifu ni mpana zaidi,
kwani vitendo vya uvunjifu wa amani na utovu wa nidhamu si vya kuvumilika
katika jamii. Kila mmoja wetu anapaswa kujua nini cha kufanya pale anapoona
vitendo ambavyo si vya kiungwana vikitendeka.
Katika siku
za hivi karibuni hususani katika mechi
za ligi kuu Tanzania bara kumekuwa kukitokea vitendo ambavyo si vya kiungwana
wala kinidhamu katika mchezo wa mpira wa miguu. Vurugu mbalimbali kutoka
mashabiki wa timu zinazoshiriki ligi kuu zimevuka mipaka kwani imefikia hatua
hata ya kurushiana mawe.Katika mechi ya hivi karibuni kati ya Mbeya City dhidi
ya Yanga mechi iliyofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kulitokea vitendo
visivyo vya kiungwana katika medani ya michezo.
Ikumbukwe
kuwa suala la ulinzi katika sehemu mbalimbali ni jukumu letu sote. Kila mmoja
wetu awe mlinzi wa mwenzake katika kuhakikisha amani na utulivu vinachukua
nafasi yake katika michezo ili kwa ujumla wananchi wapate burudani.
Vurugu na
vitendo visivyo vya kimichezo vina athari kubwa si tu kwa timu bali hata kwa
mashabiki na wananchi wa mkoa husika kwani inapotokea timu kufungiwa kutofanya
michezo yake katika uwanja wa nyumbani ni athari hata katika shughuli za
kiuchumi pamoja na kuua mapato ya mlangoni. Pia vurugu kama hizi ni athari pia
katika shughuli za uwekezaji na kuzuia upatikanaji wa fursa ya ajira kwa
wananchi.
Yapo
mapendekezo mbalimbali ya wananchi juu ya suala hili la kudhibiti vurugu katika
michezo. Itambulike kuwa ni suala la kila mwananchi kwani kama kila mmoja wetu
ataona umuhimu wa kutoa taarifa pale anapotilia mashaka mtu/watu kwa vyombo vya
ulinzi na usalama, basi suala hili tunao uwezo wa kulidhibiti na kulimaliza
kabisa.Kila mwananchi atoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha
kudhibiti na kutokomeza vitendo vya vurugu uwanjani na katika michezo kwa
ujumla.
Pengine kwa
sasa ni muda muafaka kwa uongozi wa timu pamoja na shirikisho la soka nchini ni
kuliangalia suala hili kwa kina zaidi ili kujiepusha na madhara makubwa zaidi. Kuwepo
na adhabu kali zaidi kwa timu itakayo shindwa kuwadhibiti mashabiki wake dhidi
ya vitendo visivyo vya kimichezo.
Ni imani
yangu kuwa kila mwanamichezo na wadau wote wa michezo watashiriki kikamilifu
kuzuia na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale waonapo dalili za vurugu
kutoka kwa mtu au kikundi cha watu
kikipanga njama za uvunjifu wa amani katika michezo hasa mechi za ligi kuu
zinazoendelea.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mbeya Kamishina msaidizi, DIWANI ATHUMANI anawakumbusha
mashabiki na wadau wote wa michezo kuwa “michezo ni uchumi, michezo ni
burudani, michezo ni upendo/amani na kila mmoja wetu aone kuwa ana kila sababu
ya kutekeleza hili”
UWOYA aapa kufa na kupona, kupambana na SHIGONGO baada ya kutoa siri nzito baina yao
Muigizaji wa Bongo Movie,
Irene Uwoya, ameapa kutoa siri kubwa inayofanya Mkurugenzi wa magazeti ya
Udaku, Eric Shigongo, kumchukia na kitendo kinachopelekea kumchafua kila leo
katika magazeti hayo.
Akilalamikia suala hilo ktk
post yake aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii wa instagram, amesema kwa anaye
muamini ameapa kufa na kupona kupambana na Shigongo ikiwa ni pamoja na kutoa
siri nzito inayofanya amchafue.
“Ipo siku nitaongea ukweli
kuhusu Shigongo na ushahidi ninao na nipo tayari kupigana nae hadi tone langu
la damu la mwisho” Alisema hayo Uwoya na mengine mengi.
Picha hapo chini ni jinsi
uwoya alivyotoa malalamiko hayo ambayo watu wengi wametafsiri kuwa kulikuwa na
kuombana MAPENZI kati yao.
MPYA kutoka kwa Mike T, ktk Facebook Page yake
Mike Tee ni moja kati y watu maarufu Tanzania wanaoweka Funny Post katika page zao za Face book, ikiwa ni pamoja na Masanja mkandamizaji Jana usiku Mike Tee aliandika kama unavyoona hapo juu..
LYK Movie: Kituo cha kijeshi Marekani chavamiwa, wanne wauawa
Habari kutoka Washington zinasema kuwa watu 4 wameuawa na
wengine 8 kujeruhiwa baada ya mtu asiyejulikana kuvamia makao makuu ya jeshi la
wanamaji mjini Washington na kuanza kufyatua risasi.
Habari zaidi zinasema kuwa mtu huyo bado hajapatikana ingawa
inaaminika bado yuko katika jengo hilo.
Wakuu wa kituo hicho cha kijeshi wanasema maafisa kadhaa wamepigwa
risasi na mvamizi huyo.
Polisi zaidi wamepelekwa kwenye eneo hilo huku shughuli
katika uwanja wa ndege wa Reagan ulioko karibu zikisitishwa kwa muda.
Zaidi ya wafanyakazi 3000 wanafanya kazi katika kituo hicho
kilichovamiwa. Kitengo hicho kijulikanacho kama Naval Sea Systems Command
ndicho kinachohusika na utengenezaji, ukarabati au ununuzi wa meli za kijeshi
pamoja na nyambizi za jeshi la Marekani.
Haijabainika ni vipi mtu huyo aliweza kuingia katika eneo
hilo lenye ulinzi mkali.
Subscribe to:
Posts (Atom)