Oscar Pistorius: AMUUA MPENZI WAKE

Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini Pretoria.

Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi, Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.

Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani. Duiru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu
kushiriki michezo ya Olimpiki
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.

Another NU AUDIO: Baghdad Ft. Wababa - Mpaka lini LISTEN HERE

Baghdad                                                  Wababa

NU Hit: Q CHIEF - ACCURO

Nikki wa Pili ft. G-Nako - Bum Kubam

Video mpya kutoka kwa Nikki wa pili aliyomshirikisha G - Nako Bum Kubam itazame kupitia hapa..

KIPANYA: Catoon na InfoGramme


WALTER: Ziara hii anatambulisha Album

Picha kutoka kushoto ni Walter Chilambo mshindi wa EBSS mwaka 2012,
Awaichi Mawalla (Meneja mkuu mawasiliano), Nsami Nkwabi na Norman Severino.
Washiriki wa EBSS walikuwa na mkutano na waandishi wa Habari uliofanyikia Maisha Club leo hii asubuhi kuhusu Uzinduzi wa ziara yao ya kimuziki ambapo Walter Chilambo ataachia Album yake ya kwanza katika Ziara hiyo itakayoanzia mkoani Dodoma Ijumaa ya wiki hii.

Mbeya: AMUUA MWENZAKE KISA MWANAMKE WA KILABUNI


Pic: Mfano.

MKAZI  wa mtaa wa Itiji mkoani Mbeya, Daniel Mwasalemba, ameuawa kwa kuchomwa kisu na Peter Bosco wakigombania mwanamke wa kirabuni , Elizabeth Michael.

Ugomvi huo ulianza juzi wakiwa kirabuni na ukaamuliwa na wateja wengine ambapo Peter aliondoka na msichana huyo wa miaka 18 na kwenda nae nyumbani na kumpa kichapo ambapo alifanikiwa kutoroka na kurudi kilabuni ambapo alikutana na Daniel na baadae walirudi nyumbani pamoja .

Usiku wa kuamkia leo ndio Peter alirudi ktk hiyo nyumba na kuwa kuta kisha akwafungia mlango na kwenda kutafuta kisu a aliporudi akabomoa mlango na kumchoma kisu Daniel na kumsababishia kifo

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha tukio hilo na kuwa wameukuta mwili wa marehemu kando ya barabara ukiwa uchi (bila mavazi).

Jeshi la polisi linamshikilia Elizabeth kwa mahojiano kwani Peter amekimbia na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitalini.

Barnaba - Sorry (Official Video)


Kizuri: MATUMAINI ARUDI DAR, APITILIZIA HOSPITALI

Alipopokelewa Uwanjani, Kiwewe ni msanii aliyeanza nae sanaa
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Alibebwa mgongoni kuelekea kwenye Gari
ili kwenda Hospitali Moja kwa moja.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.

BABA ASKOFU THOMAS LAISER AFARIKI DUNIA HUKO ARUSHA

BABA ASKOFU THOMAS LAISER
Baba askofu thomas laiser amefariki dunia
leo jioni saa kumi na mbili katika
hospitali ya SERIAN ARUSHA.

MGANGA WA DIOMOND AFUNGUKA: Diamond ANAENDA NJE YA MAAGANO YETU, Anguko lake laja.



Anayedaiwa kuwa ni mganga wa zamani wa Diamond, Dktari. Shehe. Yahaya amefunguka na kusema kuwa Diamond amekiuka masharti aliyompa na kuwa watu wategemee kuanguka kwake siku yoyote..

Ametiririkaaa... "Ilikuwa awe msaada kwa wengine/wasanii wachanga, anasa zimeniudhi na ilikuwa nje ya makubaliano yetu pia ni kinyume na masharti ya dawa niliyompa inayoitwa SALALA".

Alisema kuwa wasanii kama Belle 9 na Ali Kiba ndo walikuwa hit kipindi kile cha KAMWAMBIE lakini waliwazima kwa kumpa nyota hiyo Diamond. Alisisitiza kuwa kuna maagano mengi ambayo hata hayastahili kusemwa ameshindwa kuyatimiza na akimpigia simu anamuona kama adui.

Ustadh na Daktari huyo aliongeza kuwa mwanzo Diamond alikuwa anakuja kwa miguu na hata kuishia kula nyumbani kwake lakini sasa anamuona kama adui baada ya kuharibu masharti na kusema kuwa muda sio mrefu atashuka kabisa kimuziki hata yeye anajua.

Shehe, Yahaya alisisitiza kuwa hata wakikutanishwa hatasita kuongea na kuwa ataona aibu tuu, pia kuhusu Free mason alisema kuwa Diamond hayupo huko na ni uvumi anayeueneza yeye mwenyewe lakini anguko lake laja, Shehe alitaja namba yake kwa yeyote atakayetaka maelezo zaidi kuhusu hili: 0714 866416.

Vumilia - Dushe Dushe [Official Video]


RECHO - Nashukuru Umerudi Video


WALTER KUKINUKISHA DODOMA

 Baada ya kushindaMil. 50 za Epiq BSS 2012 Walter Chilambo atazunguka na washiriki wengine sita (6) wa shindano hilo mwaka jana kukinukisha Dodoma tarehe 15.

Pamoja na burudani yao watasindikizwa na Ben Pol, Barnaba, Ali Nipishe na Lina na hii ni baada ya Walter kuachia ngoma yake mpya Ijumaa hii ya tarehe 8..
Ben Pol ni moja kati ya wanaomkubali Walter pia aliahidi kufanya nae kazi..

TAARIFA YA POLISI MBEYA 05TH FEB. 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 05. 02. 2013.
 
 
WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
 
MNAMO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. AMBOKILE S/O KIKWALE,MIAKA 16,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO BAADA YA KUPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO NGUMI NA MATEKE NA MAMA YAKE MDOGO [MAMA WA KAMBO ]  BUPE W/O JOSEPH KIKWALE,KYUSA,MIAKA 32,MKULIMA MKAZI WA ILEMI  MAJIRA YA SAA 17:00HRS .CHANZO NI MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA ANAMUIBIA PESA NYUMBANI KWAKE  ENEO LA ISANGA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WATATUE MATATIZO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
 
 
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI NA KUSABABISHA KIFO
 
MNAMO TAREHE 02.02.2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LWANGWA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. IPYANA S/O SILWIMI,MIAKA 36,KYUSA ,DEREVA MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA ALIRUKA KUTOKA KWENYE GARI T.482 AYB AINA YA ISUZU ALILOKUWA AKIENDESHA KISHA GARI HILO KUMKANYAGA . MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI GARI KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA AMBAPO DEREVA ALIAMUA KURUKA  NA GARI KUMKANYAGA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KUWA NA TAHADHARI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
 
 
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI.
 
MNAO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRENK S/O HAMISI,MIAKA 25,MKULIMA,MNYIHA,MKAZI WA KIJIJI CHA CHANG’OMBE AKIWA NA BHANGI KETE 44 SAWA NA GRAM 220  . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI.TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA FAIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 
 
 
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

NU Video: Tillah - Step Out

Tizama video kupitia Infogramme, Bofya katikati kuangalia..

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA