TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS
RELEASE” TAREHE 05. 02. 2013.
WILAYA
YA MBEYA MJINI - MAUAJI
MNAMO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA SAA
18:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. AMBOKILE S/O KIKWALE,MIAKA
16,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO BAADA YA KUPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO NGUMI NA MATEKE NA
MAMA YAKE MDOGO [MAMA WA KAMBO ] BUPE
W/O JOSEPH KIKWALE,KYUSA,MIAKA 32,MKULIMA MKAZI WA ILEMI MAJIRA YA SAA 17:00HRS .CHANZO NI MTUHUMIWA
KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA ANAMUIBIA PESA NYUMBANI KWAKE ENEO LA ISANGA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA
BADALA YAKE WATATUE MATATIZO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA
MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA RUNGWE - AJALI YA GARI NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 02.02.2013 MAJIRA YA SAA
19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LWANGWA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. IPYANA
S/O SILWIMI,MIAKA 36,KYUSA ,DEREVA MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA ALIRUKA KUTOKA
KWENYE GARI T.482 AYB AINA YA ISUZU ALILOKUWA AKIENDESHA KISHA GARI HILO
KUMKANYAGA . MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA
HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI GARI KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA AMBAPO DEREVA ALIAMUA KURUKA NA GARI KUMKANYAGA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KUWA NA
TAHADHARI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA
KUJITOKEZA.
WILAYA
YA CHUNYA
- KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:30HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRENK S/O HAMISI,MIAKA 25,MKULIMA,MNYIHA,MKAZI WA KIJIJI
CHA CHANG’OMBE AKIWA NA BHANGI KETE 44 SAWA NA GRAM 220 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA
BHANGI.TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA FAIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed
By,
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment