Kiongozi wa upinzani alouawa, Mohamed Brahmi |
Tunisia inashuhudia mgomo wa taifa zima baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Mohamed Brahmi. Chama cha wafanyakazi kikubwa kuliko vyote
nchini Tunisia, UGTT, kimetoa wito wa kuwataka wananchi kupinga "ugaidi,
ghasia na mauaji"
Alhamisi polisi walitumia mabomu ya kutoa
machozi kuwatawanya waandamanaji katika miji kadhaa nchini humo, baada
ya Bwana Brahmi kuuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake mjini
Tunis.
Chama tawala nchini Tunisia, cha Kiislam cha
Ennahda kimekanusha tuhuma kutoka kwa ndugu wa marehemu kuwa kilikula
njama katika mauaji ya Bwana Brahmi.
Hii ndio hali halisi nchini Tunisia, watu wote wwaandamana. |
No comments:
Post a Comment