AFTER DEATH: Bongo Movie inayohusu Kifo cha kanumba. Check Video ya Trailer yake, maelezo na Cover Pic
Siku ya Kanumba day pale Leaders Club ilizinduliwa movie ya “After Death” kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba ambapo ndani yake kuna Jackline Wolper, Jennifer na Patrick watoto walioibuliwa na Kanumba kwenye movie na wasanii wengine wengi.
Wiki hii ndio imetoka na inapatikana kwenye maduka mbalimbali, unaweza kuitumia hii nafasi kutazama hii trailer ili upate nguvu zaidi ya kwenda kuinunua…
NIMEPEWA NA MASANJA HII
Jamaa mmoja msomi msomi kapanda bus toka Dar anakwenda Mwanza. Kwenye siti akakuta mtoto mdogo wa miaka kama 9 hivi. Kwa kuwa jamaa anajiona msomi na anapenda kudadisi akili za wengine akaona ni bora safari ikiwa inaendelea alete mada wajadili na dogo. Akaanza: Dogo hujambo? Naona unasafiri mwenyewe. Naitwa Mayala, na mimi nakwenda Mwanza. Naomba tupige stori. Unajua safari na stori ndo inaenda vizuri. Dogo akamcheki halafu akamjibu: Poa, naenda Mwanza pia. Naitwa Chale. Anza wewe stori. Jamaa akaanza: Hebu tujadili uwepo wa Mungu, hivi wewe unadhani Mungu yupo au ni stori tu? Dogo akakaa kimya kwa muda halafu akajibu: Mimi naona kabla ya kuanza kujadili hivyo, hebu tujadili hili kwanza: unawajua ng'ombe na mbuzi? Wote wanakula majani lakini vinyesi vyao ni tofauti. Kwa nini? Jamaa msomi akatafakari kwa muda halafu akajibu: Hiyo siyo fani niliyosomea. Ila sijui kwa nini. Dogo akamjibu: Sasa kama huwezi hata mjadala unaohusu vinyesi, utawezaje kujadili kitu kikubwa kama uwepo wa Mungu?
Comming soon.. G Nako, King Kikii na Joh Makini ndani ya ngoma moja
Comming soon.. G Nako, King Kikii na Joh Makini ndani ya ngoma moja.. Ni baada ya FA kutoka na wananjenje.. Mwezi ujao mapemaaaa...
HALI ILIVYO TUNISIA, BAADA YA BRAHMI KUUAWA
Kiongozi wa upinzani alouawa, Mohamed Brahmi |
Tunisia inashuhudia mgomo wa taifa zima baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Mohamed Brahmi. Chama cha wafanyakazi kikubwa kuliko vyote
nchini Tunisia, UGTT, kimetoa wito wa kuwataka wananchi kupinga "ugaidi,
ghasia na mauaji"
Alhamisi polisi walitumia mabomu ya kutoa
machozi kuwatawanya waandamanaji katika miji kadhaa nchini humo, baada
ya Bwana Brahmi kuuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake mjini
Tunis.
Chama tawala nchini Tunisia, cha Kiislam cha
Ennahda kimekanusha tuhuma kutoka kwa ndugu wa marehemu kuwa kilikula
njama katika mauaji ya Bwana Brahmi.
Hii ndio hali halisi nchini Tunisia, watu wote wwaandamana. |
EBSS A-TOWN: Hii ndio Epiq Bongo Star Search 2013 mwaka huu pande za Arusha
Subscribe to:
Posts (Atom)