NIMEPEWA NA MASANJA HII
Jamaa
mmoja msomi msomi kapanda bus toka Dar anakwenda Mwanza. Kwenye siti
akakuta mtoto mdogo wa miaka kama 9 hivi. Kwa kuwa jamaa anajiona msomi
na anapenda kudadisi akili za wengine akaona ni bora safari ikiwa
inaendelea alete mada wajadili na dogo. Akaanza: Dogo hujambo? Naona
unasafiri mwenyewe. Naitwa Mayala, na mimi nakwenda Mwanza. Naomba
tupige stori. Unajua safari na stori ndo inaenda vizuri. Dogo akamcheki
halafu akamjibu: Poa, naenda Mwanza pia. Naitwa Chale. Anza wewe stori.
Jamaa akaanza: Hebu tujadili uwepo wa Mungu, hivi wewe unadhani Mungu
yupo au ni stori tu? Dogo akakaa kimya kwa muda halafu akajibu: Mimi
naona kabla ya kuanza kujadili hivyo, hebu tujadili hili kwanza:
unawajua ng'ombe na mbuzi? Wote wanakula majani lakini vinyesi vyao ni
tofauti. Kwa nini? Jamaa msomi akatafakari kwa muda halafu akajibu: Hiyo
siyo fani niliyosomea. Ila sijui kwa nini. Dogo akamjibu: Sasa kama
huwezi hata mjadala unaohusu vinyesi, utawezaje kujadili kitu kikubwa
kama uwepo wa Mungu?
No comments:
Post a Comment