MBEYA TUNAUA JAMANI, HATUCHOKI!!

WATU wawili wamefariki katika matukio mawili tofauti, maeneo ya Ihanda na kijiji cha Nansama katika wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya.
 Katika tukio la kwanza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya alimtaja marehemu, Samweli Tensoni mkazi wa Ihanda alikutwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na sehemu mbalimbali za mwili na watu wasiofahamika.
 Alisema mwili wa marehemu ulikuwa ukiwa kwenye kalavati la reli ya TAZARA ikuwa hauna viatu na uchunguzi ulionyesha kuwa marehemu aliuawa sehemu nyingine na kutupwa eneo hilo .
 Katika tukio jingine mkazi wa Nansama, Sainesi Sampamba, alikutwa ameuawa ndani ya nyumba yake kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za tumboni na kuvunjwa shingo.
 Mtuhumiwa wa tukio hilo , Benedict Ambonisye ambaye ni mtoto wa marehemu, amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
 Chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa mashamba kati ya marehemu na mtoto huyo kwani ilidaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akitaka urithi.
 Kufuatia matukio hayo Kamanda Nyombi alisema uchunguzi zaidi wa matukio hayo unaendelea

No comments:

Post a Comment

SKILIZA & DOWNLOAD MIXING ZA DJ SPEED wa HighLands FM Radio HAPA